Jamani mafundi ujenzi nisaidieni hili.

Jamani mafundi ujenzi nisaidieni hili.

ITR

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2022
Posts
6,096
Reaction score
16,390
Nilikuwa nataka kusikimu nyumba yangu sasa nikamuambia fundi wangu anipigie hesabu ya vitu vinavyo hitajika,akapiga akanitumia picha ya vitu vinavyo hitajika.
Lakini cha kushangaza mikanda ile ya pembeni haikuwa kwenye orodha ,ikabidi nimpigie kumuuiliza nikijua labda kasahau, lakini alicho nijibu ni kuwa mikanda ni mtindo wa kizamani kwa sasa mikanda haitumiki japo kuwa ameniambia kuwa kama nataka iwepo na penyewe haina shida.

Sasa mafundi skiming naomba ufafanuzi juu ya hili ni kweli kabisa kuwa nyumba inaweza ikapendeza bila kupiga mikanda ?
 
Hata mimi fundi aliniambia hivyo hivyo kwenye bodi siku hizi hawafungi mikanda maana huo ni mtindo wa zamani.
Nikaanza kufanya uchunguzi hasa kwenye pages mbali mbali za mafundi decor nimeona wengi hawaweki mikanda na kweli inaonekana vizuri.
Nakushauri usimbishie fundi ila jipe muda wa kuchunguza.
 
Ya hata yeye kaniambia kuwa bodi inapendeza hata kuliko inapokuwa na mikanda.
 
Mm nakuambia kama fundi, achana na huo mtindo wa mikanda ni wa miaka ya 2000-2013. Tushausahau kabisa Au unajengea hela za mafao?.

Dirisha zako zina ukubwa gani?
20250126_110228.jpg
 
  • Kicheko
Reactions: rr4
Mi nilishanunua mikanda na bodi kwa hesabu ya fundi mwingine, fundi aliekuja kuskim akashauri tusitumie mikanda, nikakomaa akasema basi mikanda tuweke vymbani tuu, sa hv natamani nyumba nzima nisingeweka mikanda. Dining na sebule panavutia sana bila mikanda.
 
Yaa hata yeye aliniambia kuwa nyumba itapendeza kuliko ningeweka mikanda.
Pia aliniambia kuwa kwa sasa gibsamu zenye mapambo mengi zimesha pitwa na wakati.
 
Mi nilishanunua mikanda na bodi kwa hesabu ya fundi mwingine, fundi aliekuja kuskim akashauri tusitumie mikanda, nikakomaa akasema basi mikanda tuweke vymbani tuu, sa hv natamani nyumba nzima nisingeweka mikanda. Dining na sebule panavutia sana bila mikanda.
Angalia mfano huu
 
Attachments

  • Screenshot_20240918-170602.png
    Screenshot_20240918-170602.png
    1.1 MB · Views: 5
Eti Pendaelli nyumba bila mkanda inapendeza?
Naam inaoendeza sana, kama walivyo sema wadau kufunga mikanda ni ya kizamani kidogo, ule mvuto ulio kuwepo kwa sasa hauna maana tena.

Uzuri ni kuwa kila kunapopambazuka maboresho kwenye mfumo wa ujenzi yanaibuliwa hivyo ni muhimu kila mmoja wetu kuwa tayari kwa mabadiliko.
 
Mikanda ya juu inayotumika kuunga gypsum board na ukuta. Mimi nilifikiri mikanda ni lazima gypsum board haikai bila mikanda! Kumbe ni urembo tu
Ah ile mbona inanogesha lakini nyumba
 
Naam inaoendeza sana, kama walivyo sema wadau kufunga mikanda ni ya kizamani kidogo, ule mvuto ulio kuwepo kwa sasa hauna maana tena.

Uzuri ni kuwa kila kunapopambazuka maboresho kwenye mfumo wa ujenzi yanaibuliwa hivyo ni muhimu kila mmoja wetu kuwa tayari kwa mabadiliko.
Lakini hii sii kama mtu ataweka maurembo kwenye ceiling. Sie wape da flat ceiling sii itachukiza mzeya
 
Ah ile mbona inanogesha lakini nyumba
Ndio wanasema hapa bila ile nyumba inapendeza zaidi. Mimi naona ni preference tu sio kwamba eti imepitwa na fashion. Tatizo wabongo wanachelewa kujua vitu halafu wanaona ni mtindo mpya,ukija mtindo mwingine wanasema ule umepitwa na wakati.
 
Nilikuwa nataka kusikimu nyumba yangu sasa nikamuambia fundi wangu anipigie hesabu ya vitu vinavyo hitajika,akapiga akanitumia picha ya vitu vinavyo hitajika.
Lakini cha kushangaza mikanda ile ya pembeni haikuwa kwenye orodha ,ikabidi nimpigie kumuuiliza nikijua labda kasahau, lakini alicho nijibu ni kuwa mikanda ni mtindo wa kizamani kwa sasa mikanda haitumiki japo kuwa ameniambia kuwa kama nataka iwepo na penyewe haina shida.

Sasa mafundi skiming naomba ufafanuzi juu ya hili ni kweli kabisa kuwa nyumba inaweza ikapendeza bila kupiga mikanda ?
Fanya kitu unachopenda wewe hasa kama ni urembo au mtindo wa nyumba. Kuna watu nyumba zao zimekuwa vituko kwa kuwasiliza mafundi.
 
Back
Top Bottom