Jamani maisha magumu na kamshahara kangu nahangaika tu mtaani

Jamani maisha magumu na kamshahara kangu nahangaika tu mtaani

Wa kusoma

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2011
Posts
3,454
Reaction score
2,975
Jamani maisha magumu na kamshahara kangu nahangaika tu mtaani.

Naombeeni ushauri ni namna gani nifungue biashara ya kujikimu ili niachane na maisha ya kutegemea mshahara wadau
 
Jamani maisha magumu na kamshahara kangu nahangaika tu mtaani.

Niliweka hapa post mapema mwaka jana kwamba nimepata kazi tena serikalini na ka degree kangu lkn jamani huku maisha wacha jamani.

Na kamshahara kangu ka laki saba maisha mtaani yamebana mpaka madeni naona nilivyokuwa sijapata kazi nilikuwa huru kidogo maana sasa nina kazi majukumu kibao ukizingatia sijaoa lkn duh!
Nipeni ushauri jamani nn nifanye?
 
vumiliaaa tu mkuu....hatuna jinsi
 
Subira huvuta heri, serikalini hakuna mshahara, ila zari likikuangukia kuna DSA za kumwaga!
 
acha kufuru mwana!hujaoa unalalamika laki 7 haikutoshi!!na hiyo elimu yako unayo idhalilisha ningekuwa na uwezo ningekunyang'anya eti kadegree
 
ndugu yngu nahisi umeshaingia kwenye mikopo mapema, maaana graduate wasikuhizi mshahara wa laki tano naye anataka corola au alteza laku uzia sura kitaaa,hawajui kuwa gharama za kuendesha gari si vizuri zitoke kwenye mshaahara
 
Weka mchanganuo wa matumizi yako ....
 
mmmh kijana mshukuru mungu kwa unachokipata hakina udogo wa hiivyo kuna watu wanaishi kwa 3k sembuse 7!tafuta biashara ndogo ndogo za kusukuma kipato
 
Mbona mi nalipwa laki4na20 na nimeoa nina watoto wawili. Na maisha yanaenda vizuri? Punguza matumizi yasio ya lazima. Mshahara wa laki7 tena upo alone unalalamika? Mwenzio nina postgraduate
 
acha kufuru mwana!hujaoa unalalamika laki 7 haikutoshi!!na hiyo elimu yako unayo idhalilisha ningekuwa na uwezo ningekunyang'anya eti kadegree

Huyu analeta utani,na waalimu wa grade 111A wasemeje?,au marketing in making?

Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Natumai una maono makubwa, ni kweli hupaswi kurizika na hali uliyo nayo. Ukilizika unakuwa umeua njozi za maendeleo, Mungu ametuumba hivyo japo sisi tunachanganya kutokuridhika na tamaa. Ninachojua ni kwamba usirizike lakini uwe na furaha. Laki saba au hata milioni tano ilihali umeajiliwa wewe unaitwa bado ni mtumwa, anayepata laki nne kwa kujituma mwenyewe ni bora kuliko wewe unayetumia degree yako kupokea maelekezo mpaka juu ya maisha yako hata unapokuwa uko nyumbani bado una digest maelekezo ya mtu ambaye kwa wakayi huo yuko kwenye starehe
 
Baada ya kufikiria hivyo miaka minne iliyopita i made an instant decision to resign and create my own ways of earning money and living freely outta stress!
Ukiwa mwoga wa kuamua utaendelea kulialia milele.
 
Mshahara wako wa laki 7 hautoshi kwasababu hela hiyo ni sawa sawa na matumizi Yako jaribu kutafuta kitabu cha Rich Dad poor Dad kitakupa mwanga wa wapi unakosea na niño ufanye ila mshahara wako ni mwingi sana na unakutosha
 
Back
Top Bottom