Mshahara wako wa laki 7 hautoshi kwasababu hela hiyo ni sawa sawa na matumizi Yako jaribu kutafuta kitabu cha Rich Dad poor Dad kitakupa mwanga wa wapi unakosea na niño ufanye ila mshahara wako ni mwingi sana na unakutosha
Dada, Kiyosaki anashauri kuachana na msemo "Ishi kulingana na kipato chako" badala yake anashauri "ongeza kipato uishi utakavyo" kwa hiyo kwa mleta mada ameona mshahara huo haukidhi mfumo wa maisha yake, binafsi namuunga mkono si muda mrefu na atakuwa amechelewa akivumilia mshahara huo wakati anajua anaishi chini ya tamanio lake, bahati mbaya hawezi kujiongezea mshahara hata kama mwaka husika mwajiri kavuka lengo, kujiongezea kipato kunahitaji uhuru kamili.