Jamani mapenziii

Jamani mapenziii

Nakushauri, angalia kilichokupeleka hapo chuo ni nini hasa?Je, ni shule, mapenzi? au kutalii?
Mapenzi siku zote yapo, tena mshukuru Mungu kwamba wewe enzi hizi unawe kuomba ushauri na watu wakakushauri, enzi zetu sisi tuliharibu hakuna wa kumuuliza na unaogopa baadae ndio unakuja kujuta sana sana. Mambo haya ki ukweli yapo na hayakwepeki ila tu cha msingi ni kumtanguliza Mungu, muombe Mungu akusaidie ili akupe mke mwema mara baada ya kumaliza chuo. Na, sasa hivi soma mdogo wangu, usije juta kama tulivyojuta wengine, ukimuweka Mungu mbele yote yanawezekana.
Pole sana na Mungu atakusaidia, soma kwanza mke utampata tu
 
Kaka kwa jinsi alivyojieleza hata kama ni wa mwaka wa pili, hata akimwacha huyo akichukua mwanachuo mwingine, mambo yatajirudia yaleyale na mwishowe atashindwa shule kwani ameshasema mwenyewe anashindwa hata kusoma. WASICHANA WENGI WA CHUO WASANII!
"Mwenye masikio na asikie!" Asiposikiam ati kisa mapenzi matamu well.......Your guess is as good as mine.
Hebu fikiria kaka msichana amekuchanganya mwishowe emefeli shule, shule yenyewe ladba miaka mitatu au minne, na umri wako sasa ni miaka say 25, kwa ajili ya miaka minne basi unakubali kuharibu maisha yako kwa miaka thelathini ijayo, hiyo ni akili kweli kaka? Ushauri mzuri hata kama mapenzi matamu, avumulie, amsahau apige shule.

Tuko pamoja mkuu, ndio maana nikamwambia hilo ndilo ground la kujua haya mambo ya mapenzi, ajifunze tu kwani hata sisi tumeshapitia huko, chuo kikuu kunapatikana kila kitu, mapenzi ya kweli, ya uongo, ya mali, ya masomo (unamsomea mtu) ndo maisha ya chuo hayo, akitoka hapo amekomaa, akipata SUP pia ni part ya kujifunza.
 
mapenzi yapo na yataendelea kuwapo, na unapofanya kosa ndipo unajifunza, fanya kilichokupeleka chuoni, jichanganye kwenye mazoezi,mwombe Mungu akupe nguvu na maarifa ya kuweza kushinda kinachokusumbua
 
[B said:
kikaragosi[/B];1323340]Wana JF mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu mwaka wa pili tatizo langu mapenzi yananiumiza sana kwanza nlikuwa na mpz toka secondary tulipo karibia kuja chuo akanisaliti na sasa nipo nae clac moja japo hatongei kwakuwa anaishi na mwanaume nae tupo clac moja.Sa mwenzi wa 4 nlipata mpenzi mwingne tena mzuri zaidi kuliko wa mwanzo TATIZO nae ameanza kubadilika tena sana kutoa sababu za uongo na hata kunidanganya vibaya mno.Sijui nifanyeje na nimemweleza mambo yake habadiki na mi Nampenda staki nimwache.Plz nisaidieni maana clac sifanyi vizuri kwa Mawazo
Red:Kwa hilo jina lako...naomba nisiseme kitu!!!
 
kula shile wewe kijana achana na mambo ya love kwani utayakuta tu..
 
Unachokitafuta utakipata tu,walisema mshika mawili moja humponyoka kwa hiyo uamuzi ni wako,kaa chini ufikirie unataka mapenzi au elimu.
 
Wana JF mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu mwaka wa pili tatizo langu mapenzi yananiumiza sana kwanza nlikuwa na mpz toka secondary tulipo karibia kuja chuo akanisaliti na sasa nipo nae clac moja japo hatongei kwakuwa anaishi na mwanaume nae tupo clac moja.Sa mwenzi wa 4 nlipata mpenzi mwingne tena mzuri zaidi kuliko wa mwanzo TATIZO nae ameanza kubadilika tena sana kutoa sababu za uongo na hata kunidanganya vibaya mno.Sijui nifanyeje na nimemweleza mambo yake habadiki na mi Nampenda staki nimwache.Plz nisaidieni maana clac sifanyi vizuri kwa Mawazo
acha chuo haraka sana kabla hujadisco
 
Back
Top Bottom