Nimegundua wanawake wengi especially wenye umri mdogo ( 20yrs-35yrs) huwachukia wenzao wenye mafanikio!
Huwaongelea vibaya wenzao hata kwa mambo ambayo yapo juu ya uwezo wa mwanadamu.....
Utasikia " ana sura mbaya,mweusi kama mkaa,hana shepu,mgumba,mwembamba kama kijiti,kichwa kikubwa,sura yakiume" na mengine mengi...
Sasa huwa najiuliza hivi wewe mwenye sura nzuri,shepu nzuri,mwenye kupata watoto na n.k lini ulimpa masharti Mungu kukuumba kama ulivyo?!
Binadamu tunajidanganyaga sana..... Hakuna mtu aliyempangia Muumba aumbwe kama alivyo.
...it is just "KOINSIDENSI" kuwa kama ulivyo hivyo huna haki yakumjadili mwenzako alivyo kimaumbile.....
Nitaelewa tukilaumiana kwa vitu vilivyochini ya uwezo wetu...kama utendaji kazi,kujishughulisha na nk
Mfano ukisema "Jide ni mvivu jamani,amekaa kula tu na kipiga umbea",hapo nitakuelewa ila sio jide anasura mbaya! Sasa alijiumba yeye?
-----★★★---------★★
Binafsi nampenda sana jide coz anaonyesha njia kwa watoto wakike kwamba ukijituma utafanikiwa bila hata kutegemea kuhongwa kama wasichana wengi waleo wanavyotegemea.
Jide ametunza heshima yake kiukweli na unaweza ukaiona tofauti ya Jide na watu kama Ray C waliojiona wazuri.......
--★★----★★--★★
Ushauri.
★-★
Wasichana mwangalieni jide kama mfano kwenu,acheni majungu na kumjaji jide vibaya.....
★UZURI UPO MOYONI KWA NJE MNAJIONGOPEA★.
Na kwa JIDE namwambia piga kazi kama kawaida yako,binadamu tuache tupige kelele tujifariji na umaskini wetu....
Usitushangae ni katika njia ya kujifariji na ugumu wa maisha ndo tunapokujadili jadili.★....