Jamani mnaingizaje hela kwa siku? Tupeane hiyo michongo

simba wa dodoma

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2017
Posts
928
Reaction score
1,012
Mambo vipi wadau,

Mimi kijana nafanya kazi sehemu moja ila mshahara wangu mdogo ila unagawanyika sana naona kabisa mshahara haujitoshelezi. Nimeandika huu uzi kwa wale wajanja mjini tupeane basi code nasi tufanye hizo harakati tutoboe wote maisha kiukweli hela ya kutegemea mshahara ni mateso sana.

Kama una mchongo mzuri tuambieni ila sio wale business networking huko pasua kichwa maana kuna ndugu yangu alishawahi kufanya mwishoni kaishia kuacha tu na kawa maskini.

Tusaidieni na mimi nimiliki nyumba na magari.
 
Bado sijatoboa, ila watu wasema" pesa wanazo masikini wa mtaani kwenu" hili ni fumbo ukiweza kulitegua utapata pesa nyingi tu,..... MO na bakharesa wameweza kutegua na ndio maana biashara zao wamewalenga watu masikini. Mfano MO anauza juice ya ukwaju 300, lakini anatengeneza pesa mbaya, hauzi juice 5000, kwa maana matajiri hawana pesa za kumfanya akawa tajiri. Tafakari CHUKUA hatuaa.....haki pesaaaaaaa, gwe gwe gwe
 
Utajiri ni kuangalia tatizo linaloizunguka jamii yako na kulitafutia ufumbuzi mfano kama sehemu unayoishi kuna shida ya maji basi hapo biashara ya maji ni fursa. Kama unapoishi kuna shida ya unga wa ngano basi hiyo ni fursa.

Kama unaona watu wananunua mafuta ya bodaboda kwa kutumia chupa za maji basi hapo hata ukiweka pampu moja ya petrol unatoboa.

Ukiona hamna sehemu ya kuangalizia mpira jua hiyo ni fursa. Usiige wanachofanya wenzio mfano ukaona masaki wanakunywa sana huisi ukaanzisha biashara hiyo Kwa mtogole. Kule wana mahitaji tofauti
 
bado sijatoboa,ila watu wasema" pesa wanazo masikini wa mtaani kwenu" hili ni fumbo ukiweza kulitegua utapata pesa nyingi tu,..... MO na bakharesa wameweza kutegua na ndio maana biashara zao wamewalenga watu masikini.mfano MO anauza juice ya ukwaju 300, lakini anatengeneza pesa mbaya,hauzi juice 5000, kwa maana matajiri hawanapesa za kumfanya akawa tajiri. tafakar CHUKUA hatuaa.......haki pesaaaaaaa,gwe gwe gwe

Africa wenye kipato kidogo na cha chini ni wengi, hivyo ukifanya biashara kuwalenga hao na ukawa mvumilivu kwa kukusanya miamia zao kwa muda mrefu lazima utoboe.

Lakini pia siku zote Production inalipa kuliko uchuuzi, hawa akina Mo na Bakhressa wamejikita sana kwenye production na hili liko sana na kwa hawa wenzetu wahindi na waarabu..
 
Africa wenye kipato kidogo na cha chini ni wengi, hivyo ukifanya biashara kuwalenga hao na ukawa mvumilivu kwa kukusanya miamia zao kwa muda mrefu lazima utoboe.
Lakini pia siku zote Production inalipa kuliko uchuuzi, hawa akina Mo na Bakhressa wamejikita sana kwenye production na hili liko sana na kwa hawa wenzetu wahindi na waarabu.

Best yangu production kibongo bongo ina ukiritimba sana!..ndo maana wachache wanatoboa.
 
bado sijatoboa,ila watu wasema" pesa wanazo masikini wa mtaani kwenu" hili ni fumbo ukiweza kulitegua utapata pesa nyingi tu,..... MO na bakharesa wameweza kutegua na ndio maana biashara zao wamewalenga watu masikini.mfano MO anauza juice ya ukwaju 300, lakini anatengeneza pesa mbaya,hauzi juice 5000, kwa maana matajiri hawanapesa za kumfanya akawa tajiri. tafakar CHUKUA hatuaa.......haki pesaaaaaaa,gwe gwe gwe
Nashangaa wajasiliamari wetu, unakuta anauza mfano mafuta ya Nazi 15000, kichupa kidogo, yaani Bei inazidi bidhaa ya hivyo hivyo kutoka China.
 
bado sijatoboa,ila watu wasema" pesa wanazo masikini wa mtaani kwenu" hili ni fumbo ukiweza kulitegua utapata pesa nyingi tu,..... MO na bakharesa wameweza kutegua na ndio maana biashara zao wamewalenga watu masikini.mfano MO anauza juice ya ukwaju 300, lakini anatengeneza pesa mbaya,hauzi juice 5000, kwa maana matajiri hawanapesa za kumfanya akawa tajiri. tafakar CHUKUA hatuaa.......haki pesaaaaaaa,gwe gwe gwe
[emoji38][emoji38][emoji38]nimekukubali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliwahi fikiria kutengeneza wine ya strawberry ...vizingiti mob!
Ooh ok, kwa huko ni pazito , Kuna family member yeye alikua na kiwanda cha sembe..Kuna wakati nilisimama kiwandan kwake hapo , aisee.. biashara ilikua imenyooka mno , kaja kujichanganya mwenyewe baadae..mambo mengii wakati bado hajawa mkubwa ile ile..kaanguka, ndio anaanza tena

Kajichanganya kiaje? au aliidhamini Yanga akafulia? au alianza hizi siasa uchwara za bongo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ooh ok, kwa huko ni pazito , Kuna family member yeye alikua na kiwanda cha sembe..Kuna wakati nilisimama kiwandan kwake hapo , aisee.. biashara ilikua imenyooka mno , kaja kujichanganya mwenyewe baadae..mambo mengii wakati bado hajawa mkubwa ile ile..kaanguka, ndio anaanza tena

Sent using Jamii Forums mobile app

Ah kuwa na kiwanda cha sembe very easy
 
Back
Top Bottom