Enzi hizo Tanzania tulikuwa na kituo kimoja cha radio, RTD. Piga ua ilikuwa lazima tu usikilize vipindi vyao vile vya ajabu ajabu kama vile,
1. Mbiu ya mikoa
2. Asilia salamu
3. Ukulima wa kisasa
4. Fimbo ya mnyonge
Nakwambia ilikuwa shughuli haswa, mwenye kukumbuka vinginvyo aongezee.
Hii niliirushaga michizi blog sometimes 2008 watu wakilumbuka mbali sana
(link hii hapa kwa comments jamaa walizotoa
http://issamichuzi.blogspot.com/2008/11/vipindi-vya-rtd-unavikumbuka.html)
Vipindi Vya RTD Unavikumbuka??
Wadau leo nimeona nije na hii nyingine, nimekumbuka sana ile miaka ya nyuma kidogo wakati tulikuwa hatuna radio stations nyingi kama zilivyo sasa, wakati huo station ilikuwa ni Radio Tanzania tu na ile idhaa yake ya kiingereza (External).
Fashion ya radio ilikuwa ni zile wanaita RADIO MKULIMA na brand names zake zilikuwa ni NATIONAL Panasonic ama PHILIPS. Mzazi alikuwa anainunua RTC (yale maduka ya uma).Tukirudi katika vipindi, navikumbuka sana vipindi vifuatavyo ambavyo bila shaka mdau utakubaliana na mimi vilikuwa maarufu kutokana na zile nyimbo za utangulizi kuashiria kipindi kuanza ama kumalizika.
"Sikiliza Bwana Umeme... (Bwana Umeme) - Kile kipindi cha TANESCO cha kuelimisha umma kuhusu matumizi mazuri ya umeme.
"Starehe na BP " - Uncle J. (Julius Nyaisanga) alikuwa anakimudu vyema kabisa""Kahawa ni Mali" - Namkumbuka sana yule mama wa kiashirio cha kipindi akitamka hayo maneno kwa rafudhi ya kichaga.
"Jifunze Kiswahili Fasaha" - sina uhakika kama nimeandika vyema tittle yake lakini kilikuwa ni kile kipindi kizuri kilichobuniwa kuhamasisha watu kuzungumza kiswahili katika harakati ya kuwaunganisha watu wa mikoani na wa Bara. Nakumbuka kiashirio chake kuna sehemu inasema.. na mikoani... ni kiswahili chatumika.....Bila kusahau vipindi kama..
"TTCL Simu kwa Maendeleo" kipindi cha "Serikali za Mitaa", " Afya yako /Afya ya jamii " sikumbuki vyema title ila nakumbuka kiashiria cha kipindi ulikuwa ni wimbo mmoja anaimba Kept John Komba na kundi lake wakati ule.
Ukija vipindi vya week ends kama "Club Raha leo Show", bila kusahau kipindi cha "Mama na Mwana" namkumbuka mtangazaji Edda Sanga alikuwa anakimudu vyema kipindi na zile hadithi za "Adili na Nduguze", "Kisa cha Mfalme Juha", ile hadithi ya watoto wa mfalme wanakwenda kutafuta wachumba wa kuoa... n.k wadau ongezeeni hapo kumbukumbu zenu.
Japokuwa kilikuwa ni kipindi cha watoto lakini nakumbuka watu wazima walikuwa wanazifuatilia kwa umakini sana zile hadithi bila kukosa sehemu hata moja juma moja baada ya lingine.
Wakati ule radio ilikuwa na msaada mkubwa kuelimisha jamii nzima (wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara) kuhusu mambo mbali mbali na watu walikuwa wanafuatilia sana.
Je, wewe mdau unakumbuka nini miaka hiyo hapo kunako Radio Tanzania (RTD)???
Mdau yule yule wa Dodoma,
Natanguliza shukrani Bro Michu
© Michuzi | Friday, November 14, 2008 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako |
Maoni: 92
Tarehe Fri Nov 14, 02:32:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
Hapo mdau kasahau asubuhi tunaamka na MAJIRA. tunapata habari toka kwa wawakilishi mikoani. Kuna kipindi nilikuwa nakichukia sana kwa sababu kikianza tu nasikia njaa MALENGA WETU. Vipindi vingine kama JENGA NA MECCO,TAIRI GENERAL na marehemu bati kombwa, Kipindi cha Michezo saa mbili kasorobo. YOTE TISA KUNA KIPINDI NAKIMISI SANA. 'MUZIKI NA HISIA' Kipindi hiki kilinivutia sana. Wadau lete vipindi vingine
Tarehe Fri Nov 14, 03:24:00 AM, Mtoa Maoni: Mkazi Wa Makojo, Mara
Ilikuwa myeyusho tu, sisi kwetu tulikuwa tunapata mawimbi ya sauti ya Kenya kuliko RTD na kipindi alichokipenda sana mama yangu ni 'JE HUU NI UUNGWANA?'NA MAMBO MBOTELA!
Tarehe Fri Nov 14, 03:30:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
Mie naukumbuka ule wimbo wa mzee Makongoro akiwaonya madereva wasinywe kileo kama gongo na kuendesha. 'Ati dereva kalewa gongo ah! sawa hiyo?!' Halafu wengine wanabwakiza 'haata hiyo si sawa dereva acha vitukoo!!. Wimbo huu ulitungwa kufuatia hotuba ya mwalimu Nyerere akiwaonya madereva kuwa wastaarabu barabarani. Hiyo ndiyo ilikuwa miaka ya chama kimoja chenye uongozi thabiti wa Taifa.
Tarehe Fri Nov 14, 03:31:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
Duu hapo umasahau kulikuwa na mchana mwema, wahenga wetu,wakati wa kazi, mazungumzo baada habari, mambo mpwitompwito,pwagu na pwaguzi,kumakucha jamani kumekucha,from me to you, dial a disc,majira na zengine kibao nipe muda nitakulretea.
Tarehe Fri Nov 14, 03:51:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
Mdau kuna na hivi vifuatavyo:
Kijaluba, Kipindi cha Mashairi
Pwagu na Pwaguzi.
Bila kusahau kipindi ambacho kwa sasa hivi kingekuwa na kazi ya ziada cha Mikingamo. "Ndugu fulani wa jiji fulani akishirikiana na fulani walikwiba pesa za umma na kuzificha kwenye kisiwa fulani!"
Tarehe Fri Nov 14, 04:02:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
Duuuuh mdau wa dodoma umenikumbusha mbali sana na kipindi cha hadithi ''KISA CHA MFALME JUHA'' kwani nilikuwa sikikosi hata kidogo zile hadithi nakumbuka niliachwa na treni kwenda Dodoma kwa kumalizia kipindi ikabidi nisafiri siku nyingine. Kweli ya kale Matamu
Tarehe Fri Nov 14, 04:14:00 AM, Mtoa Maoni: Halikuniki
Mdau kipindi cha mama na mwana hapo zamani kilikuwa kinaendeshwa na DEBORAH MWENDA!Wakati huo hadithi ya Binti chura na Ua jekundu zinatukusanya pembeni mwa redio kuanzia saa 8 mchana.
Any way.. kila mtu na zamani yake, hata mtoto wa mwaka mmoja nae ana zamani yake!
Binafsi nakumbuka kipindi cha Mzee jangala cha usiku, kilikuwa kinadhaminiwa na "CHIBUKU"
Zaidi ya yote kipindi cha jumapili salamu za wagonjwa hospitalini. Kiashiria ni wimbo wenye ujumbe mzito " ..Ajue bwana mungu wa mzima kuwa mfu mgonjwa kuwa salama..."
Mwisho sikisahau kipindi cha majira asubuhi saa 12.30 kilikuwa kinanikera sana sababu ndo mida ya kuwahi namba shuleni (shule ya msingi Tandale Dar.), viranja wanoko na mwaalimu wa zamu balaa ukichelewa namba. Huku nimebeba dumu la maji ya kumwagilia bustani za shule, huku ufagio wakufagilia, huku kifuu cha kupikia uji wa shule, huku nimebeba madaftar, huku michongoma sijui yakueka kwenye uzio, huku kikombe cha uji..dah kama askari anaenda vitani!
Ah imebaki historia wala haijirudii tena...!
Tarehe Fri Nov 14, 04:17:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous
(Ugua poe )JUMAPILI.wakati umewadia wasalamu kwawagonjwa hosipitalini leo tunawapa pole.....
Mikingamo.Asiria salam.Malenga wetu,Jumanne kibao.Tumbu