Jamani mnalikumbuka hili!.

Duh! Mimi nakumbuka kipindi cha Mikingamo!!!!
".....bimu limeshapasuka, wakanguzi wanahangaika, wahujumu wanatapatapa....."
Yaani bana... Mafisadi yalikuwa yanitwa na kujieleza kwenye radio mali walizonazo na walikozipata! yaani ilikuwa kazi kwelikweli kwa mafisadi enzi hizo!! hasa ukikamatwa na mche mmoja wa sabuni aina ya kanga

Hata hivyo kilikufa mzee wa "hekima na msuluhusha migogoro alipoingia madarakani..... Mashangingi yakaanza kuota kama uyoga!!!!
 
wakuu mnakumbuka maigizo ya Mzee Jangala usiku saa tatu???, never miss.
enzi hizo kwanza mwasikiliza wadhamini CHIBUKU!!, ..chibuku oyeee, chibukuuu hongera hongeraa hongeraaa...!, duh.

duu umenikumbusha mbali, tumia chibuku ni pombe bora tumia chibuku ni pombe boraaaaa. Jangala, kiatu (thiyo hivyo), Mzee Mundu na wenzao
 
...'mixed grill' RTD External service kila jumapili mchana...acha tu, enzi hizo 'bumping' kwenda mbele, Carl Douglas na Kungfu fighting 🙂

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=jhUkGIsKvn0&feature=related[/ame]​
 
Na ile michezo ya redio ya akina Jangala? (Chibuku) Ilikuwa famous kweli kweli, ukimiss ni kama vile umemiss komedi! Teh teh teh!
 
Kulikuwa pia na Abdul-Omar Masoud, na kile kipindi cha Michezo. Wakati fulani akadokeza ule mziki wa kuanzia na akaukata kwa hafla na kwa furaha akasema- Lisemwalo lipo kama halipo laja- Yanga Bwanga aingia Yanga.
 
Daaaah si mchezo ndugu, enzi za 'kilimo cha kisasa' nlikuwa nasoma makuyuni jkt
sekondari, ebwanae tulikuwa na mashamba lukuki, lazima tukapalilie asubuhi kuanzia saa 11 hatua 4 kwa 180 ndo tuende darasani, mkuu wa shule alikuwa masai mkali kama nyuki lazima uamke uende au utapewa nusu heka mwenyewe jioni. mnakumbuka majira? kawimbo kakeje?
 
Mimi mpaka leo nataka kujua aliyepiga zile nyimbo za MAJIRA,MCHANAMWEMA na MICHEZO na wapi ntapata records zile.Alipuliza trumpet vizuri and drums arrangement zilikuwa bomba.
 
Mimi mpaka leo nataka kujua aliyepiga zile nyimbo za MAJIRA,MCHANAMWEMA na MICHEZO na wapi ntapata records zile.Alipuliza trumpet vizuri and drums arrangement zilikuwa bomba.

Na ule wa Jioni njema mkuu. wimbo safi sana ulee
 
Aah! long time kitambooooooo!!!!!!!! mi numekumbuka CLUB RAHA LEO SHOW!!!! na

Uncle J. NYAISANGAH watu wanachemka kisawasawa.
 
Pia kulikuwa na kipindi cha kijaruba kwa kina dada, kwa kuwa radio ilikuwa moja hata sisi kina baba tulikuwa tunasikiliza ubeya wa kina mama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…