Jamani msaada tafadhali

Maiga

Member
Joined
Oct 22, 2011
Posts
59
Reaction score
3
Mdogo wangu sikio linamuuma, anadai akitafuna kitu anapata maumivu.

Anahis kuna kitu kinatembea na kwa kweli anahiis maumivu mpaka analia. Jana usiku hakulala kabisa, nimemnunulia dawa ya drop kama huduma ya kwanza lakin anadai bado anaumia.

Naombeni msaada wenu ,wakubwa nawasilisha.
 
dah pole sana
hiyo dawa sio sahihi kuitumia bila ushauri wa daktari,,,,,inaweza kwenda kuongeza au tatizo au kuzua tatizo jingine

nakumbuka nikiwa std six niliwahi kuumwa sikio nikawa nalia kama mtoto alipita babu mmoja akanipa kopo ananiambia kakojoe mkojo humu nikakoko huku nalia akamwambia mdogo wangu aumwage abakishe tone kisha umwekee mwenzio sikioni. akaniwekea ndani ya dk2 nilipona hadi leo sijawahi umwa sikio
 
Pole sana kwa dogo.
Kuna dawa huwa inaidia sana ni mafuka ya kuku,Kama unaweza pata kuku ukamchinja kuku mwenye afya i mean mnene ndo huwa na mafuta.After kumchinja toa mafuta mafuta yeyusha then yawe ya vuguvugu mwekee dogo kwenye sikio linalouma ama yote atapona mara moja na halitorudia kwa the same chanzo.kama utaweza ni njia nzuri japo pia waweza kwenda hospitali.
 
So unashaur na yeye afanye hvo!.mi kwa haraka nilijua ni vidonda, !ndo maana nikamchukulia ile drop.
 
Mwenye kujua chaanzo nin anisaidie, pi naendelea kupata mawazo ya nin kifanyke
 
Pole sana mkuu.
Binafsi siwezi kucoment kwenye dawa za kienyeji,ila nachowezasema ni kwamba dawa nyingi za matone sio salama kwa sikio la namna hiyo.Kuna tatizo linaitwa Acute Otitis Media inawezeka ndilo mdogo wako analo.

Bahati mbaya hujasema mdogo wako ana umri gani na ameanza lini kuumwa.Pengine ungetuambia hayo ili tuone jinsi ganitutakusaidia. Ila nina wasiwasi na uwezo wa kitabibu wa huyo aliyewauzia hiyo dawa. Nadhani alitakiwa kwenda mbali zaidi ya hapo.

Kama una dawa yoyote ya maumivu hapo ndani mpatie badala ya hiyo ya matone.
 
Ana miaka 22.na kaanza jana jioni

Kama uko karibu na duka la dawa mnunulie Ciprofloxacin 1x2 kwa siku tano na Diclofenac 1x3 kwa siku tatu. Naamini zitamsaidia.
 

Ni vizuri zaidi ungepata kuku wa kienyeji.
 

hii ni kweli kabisa, juma lililopita niliumwa sikio la kulia nkanunua ear/eye drops haikufanya kazi
nikaambiwa nitafute mafuta ya kuku.....nakuambia matone mawili niliweka usiku mpaka asubuhi nilipona 90%. Nikaweka mara ya pili asubuhi likapona kabisaaa baada ya masaa
matano. Huwezi amini mafuta ya kuku ni dawa ya ajabu.

Ukishayaweka ulale upande ili yasitoke. Uwekwe na mtu
ukiwa umelala
 
Kama mkuu ametuelewa nadhani atamsaidia mdogo wetu.
 
leo kdogo kapata ucngzi ,thanks sana waungwana, nimefata mawazo yenu na leo tunaenda hosptali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…