Habari zenu wana jamvi. Naombeni msaada wenu,nina mdogo wangu yapata miezi 6 sasa anateseka na ugonjwa wa u.t.i. Nimeshampeleka hospitali na kashatumia vidonge vingi bila mafanikio. Kikubwa anacholalamika ni maumivu chini ya nyonga kuzunguka mgongo mpaka ikanibidi wiki iliyoisha nimpeleke m/nyamala akapige utra sound.Majibu yake ni kwamba hana tatizo la kibofu ila kuna vijidudu vimeenda kushambulia njia ya kizazi.Sasa sielewi nimsaidiaje maana anateseka na kila akipima mkojo bado mchafu.Nifanyeje?