Shikamoo Babu,
Baada ya salamu napenda kujua kama mzima wa afya mimi sijambo huku mjini wote wazima kabisa natumaini bibi yangu hajambo yule mbuzi bibi aliyenipa ameishaanza kutoa maziwa? Nikija kijijini nitakuja nimchukue nimlete huku mjini nipate kumfuga vizuri babu huku mjini kuna magari mengi sana sio kama kijijini halafu kuna umeme na video na kuna taa barabarani mji ni mzuri kweli babu nitakutumia nauli uje huku unitembelee.
Babu ile baiskeli yangu ilikuwa na matatizo ya spoko nakumbuka niliiacha kule kwenye migomba huku baiskeli ziko nyingi nitakutumia na wewe ya kwako yule mchumba wangu mtoto wa jirani yetu Shemdoe yupo? Msalimie sana babu.Babu naomba ukimaliza kusoma hii barua umpe na bibi naye asome nimeweka humo noti ya elfu kumi kwa ajili ya ugoro wako nahisi utakuwa umeisha.
Nikipata nauli nitakuja.
Mjukuu wako mpendwa
The Finest.
Ahsante sana TF,
I really shed my old tears! Umenikumbusha mbali mjukuu wangu.
Sote tuko wazima ikiwa ni pamoja na yule mbwa wetu, watoto wake na yule wa jirani yetu aliyemzalisha. Mbuzi wetu wate wazima, wanatamani kukuona. Yule bibi wa mtoto tuliyekupa amajifungua mapacha watatu. Yaani tayari ni wengi mno kiasi kwamba nashindwa kuwapeleka marishoni. Hata hivyo watoto wa jirani yangu (wale mliocheza nao siku ile) wananisaidia. Kuku nao ni wazima. Bata hao usiseme. Baba zako wakubwa na wadogo hawajambo. Wanasema uje kuwaona tena usichelewe. Bibi kachoka ila bado anaweza kwenda kwa jirani yetu (siyo yule mchawi) kuomba moto! Mama wadogo nao....Shangazi pia......Ohhhhhhhhhhh, nimesahau jirani zetu...
Asante sana kwa kutukumbuka na kututumia pesa. Usiache kutukumbuka sisi wazee wako.
Wako akupendaye,
Babu DC