Jamani naombeni ushauri, haya malalamiko yangu niyapeleke wapi????

mito

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2011
Posts
10,682
Reaction score
10,801
Wakuu nimeagiza zana fulani hivi za kijasiriamali toka nje ya nchi. Mzigo umeishaingia bandarini siku nyingi (hii wiki ya 2 sasa) ila sijafanikiwa kuutoa kwasababu ya vikwazo ninavyokumbana navyo toka kwa wakala wa meli wa Dar.

Supplier (jamaa walioniuzia mzigo) walinitumia copy ya Bill of Lading nikampa clearing agent wangu aendelee na mchakato wa kutoa mzigo. Supplier alisema ameishatoa release hiyo niendelee na procedure za clearance meli ikiwasili nitapewa mzigo wangu. Pia nilienda kwa wakala wa meli kupata confirmation meli inawasili lini. Nilimuonyesha zile shipping docs na yeye nikamwachia copy, then akasema haina shida nimpe muda afanye mawasiliano kujua meli inawasili lini. Hapo akanipigisha tarehe wee hatimae meli ikawasili.

Sasa clearing agent amefikia hatua anataka release ya mzigo toka kwa wakala wa meli. Hapa ndo kizungumkuti kilipoanzia hadi sasa wiki 2 zinakatika wakala hataki kutoa release. Anadai sawa docs zangu zinaonyesha nimelipia freight lakini za kwao hazionyeshi hivyo, so hawawezi kutoa release. Kinachoniudhi ni kwamba huyu wakala amekaa nacopy za docs zangu mwezi mzima, na zimeandikwa nimelipia kila kitu, iweje leo hii ndo anaibuka na kikwazo hiki? Matokeo yake sasa mzigo wangu umeishaanza kuhesabiwa storage charges!

Mbaya zaidi ananiambia niwasiliane na shipper wa mzigo wangu nimwambie awatumie email kwamba nimelipia kila kitu watoe release ya mzigo. Ninachojiuliza wao ndo mawakala wa hiyo meli kwanini hataki kuwasiliana nao moja kwa moja?? at the same time nikiwapigia shippers wanadaie wao walishatoa release, hapo ndo nachoka!

Wakuu naombeni ushauri khs cha kufanya ili nipate mizigo yangu manake storage charges zinazidi ku-accumulate!!
 
Kwani bei gani wanataka uwalipe? Ninavyofahamu Mimi shipping line agents lazima uwalipe kiasi fulani hapa bongo, hizo ni hela tofauti kabisa na freight charges mliokwisha lipa. Sasa bosi ni bora ulipe mapema utoe mzigo wako otherwise utashindwa kuutoa storage charges zinapozidi kuongezeka. Sifahamu wapi unaweza kwenda kulalamika, lakini wasiliana na clearing agent mwingine akupe maelekezo nini cha kufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…