Naomba ushauri jamani,yani mvua ikinyesha naumwa sana vichomi na pia nabanwa na kifua sana,lkn leo kiuno kinaniuma sana hata sijui tatizo ni nn,nisaidieni
Pearl, pole sana. Sio ajabu mvua ikinyesha kuandamana na watu kadhaa kukumbwa na mafua, kubana vifua, vikohozi na homahoma. Ijulikane kwamba mvua hutibua mavumbi na vimelea kutoka chini na kuifanya layer ya chini ambamo tunaishi na kuvuta hewa yake iwe nzito na iliyotibuka. Mwili nao umeumbwa kwa ustadi kupambana na hali korofi kama hizo. Hewa iliyotibuka kupata pingamizi kutoka mwilini ambapo puwa huwa na kazi ya ziada kuchuja taka na kuekebisha ujoto sahihi unaoweza kustahimilika na mapafu ambayo ni dhaifu. System nzima ya hewa hubadilika kuhimili mabadiliko hayo na ndio mana tabaka la juu "mucosa layer" ya respiratort tract huongeza utando wa mucus ili kunasa tabaka chafu linalopenya kwenye hairy nose. Ex-peristalsis huchukuwa nafasi ambapo wakati nywele za puani huswaga uchafu ulionaswa na kuzamishwa kwenye kamasi iliyotengenezwa kwa uoshwaji huo, mucosal fluid nayo kutoka chini zaidi ya njia ya hewa huswaga uchafu kuelekeza mdomoni na puani ili ukohoe na kutema as a reflection.
Wale watu ambao reaction yao huwa ya kishindo kwa gene zao, huathirika zaidi kwa sababu threshold zao za kuchukuwa hatua huwa chini zaidi na hivyo kushituka haraka zaidi - allergic to allergens - HYPERSENSITIVE. Ndio maana watu hao hata mawingu tu yakitanda wao hubanwa vifua vyao (PUMU), mvua ikinyesha wao hudhurika upesi. Lakini Threashold za watu mbalimbali zinatofautiana, kwa hiyo mwingine mwili wake unapambana na hali na hatima yake huishia kwenye mafua tu mapesi, wengine kama immunity pia ipo chini mafua (URTI) huendelea hadi kuwa descending RTI ambapo atakohoa na mwili kupanda joto kiasi kwamba wengine hudhania ni malaria.
Ufanyeje sasa? Kwa kawaida ni vema kujua ni nini chanzo cha tatizo lako. Ukiwa unajiangalizia, chukuwa ndimu kamulia kwenye maji na kunywa au nyonya juisi ya ndimu au limau mara kwa mara. Unaweza kutumia ndimu iliyokaushwa inapatikana kwa wauza viungo vya chakula sokoni - vinafanana na chumvi. Unaweza kunywa chai na tangawizi au maji moto. Hivyo husaidia kufungua mishipa ya damu ya njia ya hewa ili kuupa mwili uwezo kuondosha vichokozi, lakini pia maji dawa mwilini kwako kuongeza mzunguko na kusafishia sumu mwilini unaosha kwa kukojoa sumu iliyo mwilini. Kama kichwa kinauma tumia paracetamol (panadol) au dawa zinazofanana na hiyo, sio mbaya piriton ikitumika pia.
Kama kuna kikohozi, kuna dawa nyingi mno za kikohozi ambazo zimekuwa na mchanganyiko wa vitu kwa tiba mbalimbali, mfano muolyn, Koflyn ambazo zina piriton pia na kadhalika. Dawa yenye mchanganyiko mwingi zinafaa zaidi. Kama kifua kinabana zaidi unaweza kupata dukani kwa madawa salbutamol ikakusaidia, kidonge shillingi 10 kwa sasa, aminophylline na kadhalika vyaweza kusaidia. pale dukani watakupa ushauri wa dawa inayokufaa zaidi.
Ukiona hali mbaya inazidi, mwone daktari au mganga. Usikimbilie antibiotics mpaka daktari au mganga amekushauri hivyo, maana ukiianza doseya antibiotics ni amri uimalize at least kwa siku tano kuzuia resistance.
Kiuno na viungo vingine mara kwa mara hujionyesha wakati huo wa mafua, lakini vyanzo vingine vipo ambapo daktari ukikaa naye kumsimulia akakudadisi na kupima atagundua tatizo na kukupatia namna ya kudthibiti. Yawezekana kutoka hapo ukaangalia upana wa vianzo vya matatizo, vingine ni vidogo sana utashangaa, usijejaribu kumpiga mbu kwa kombora la masaafa marefu kumbe hata kofi lako tu lilitosha kummaliza. Upo Pearl? Pole tena.