Saluti mkuu,hiyo ni sawa kabisa nimekubaliana na wewe lakini hii microfinance inachallenge zake kubwa,nakumbuka kuna mama alichukua mkopo hukohuko microfinance ilikuwa kitu kama laki 8,akaziingiza kwenye biashara zikazama akashindwa kulipa interest ikaongezeka mpaka akawa anadaiwa 2m wakaja nyumbani kwake kumsafisha vitu vya ndani ikawa vurugu mme wake akaweka ngumu pigana peleka polisi,kesi,na vitu vya ndani ya nyumba hawakupata hela yao ambayo ilikuwa imeshafika 2M hawakulipwa bado kuuzuria mahakamani sasa vurugu zote zinanifanya mie naona hii issue ya microfinance kuifanya lazima uwe na thick skin.
Suala lingine ni hiyo interest ya 10 to 30 percent per monthy sizani kama ukiiandikisha microfinance yako kisheria unaruhusiwa kuweka interest unayotaka wewe lazima kutakua na baseline.
Nawasilisha.
Wakati ninakubaliana nawe kuwa biashara hii ya mikopo in challenge zake, ni vyema tukakubaliana kuwa kila biashara ina challenge zake pia. Nirudi hapo kwenye baseline unayoizungumzia, ni kweli kuwa BOT inaweka viwango vya chini na vya juu vya kutoza riba katika Taasisi za kifedha, lakini jiulize wangapi wanajua? Je wanafuatilia? Mara ya mwisho nilipopata data za viwango vya riba ilikuwa kama 24% per annum kama nakumbuka vizuri which is equal to 2% per month.
Wakati huo huo nilipoenda Access Bank na Advance Bank nikakuta wanatoza riba 5% per month (which is equal to 60% per annum;- reduced, yaani riba inakokotolewa kulingana na principal ammount inavyopungua).Nilipoenda FINCA ninakuta watoza 3% per month (which is equal to 36% per annum:- huku ni flat rate yaan hata principal amount ikipungua mpaka laki moja kutokana na marejesho bado utalipa interest ya principal amount uliyochukua awali i.e 10m) BOT wako wapi hapo?
Sasa ni vyema tukaelewa tukazigawa hizi taasisi za mikopo katika makundi mawili: 1. zile zinazochukua akiba kutoka kwa public na 2. Ni zile sizizochukua akiba. Hizi zinazochukua akiba kama mabank ndizo zinazokuwa regulated na BOT. Sasa jiulize kama mabenki yanakuwa regulated na yanaweza kutoza riba wanazotaka je tuna regulatory framework nchi hii? Au ndio REGULATORY CAPTURE? Au ndio CONSPIRACY OF THE RICH? Mi sijui!
Ok hayo tuyaache, turudi kwenye biashara yetu ya mikopo. Sasa kwa kuwa tumekubaliana kuwa taasisi hizi hazichukui akiba kutoka kwa Public, inamaana haziwi regulated (
Ndio lengo la ile hoja binafsi sijui ni ya Makamba) sasa kila mtu anajiamualia anavyotaka (
si unajua soko huria). Lakini ukitaka uoperate formally ni lazima upate kibali kutoka BOT, but kutokana na mtaji unaohitajika ili upate hicho kibali wengi wanashindwa kuvishughulikia. Kuhusu kama BOT wanaruhusu riba hizo za 10% jibu ni NDIYO. Kuna jamaa yangu aliweza kupata hicho kibali baada ya kukidhi matakwa ya mtaji unaohitajika na sasa anatoza riba ya 10%. Hao wanaotoza riba ya 20% na 30% kama wanaruhusiwa siwezi nikasema kwa sasa, kwani wengi ninao wafahamu wanaoperate informally.
Talking about informal operation: Ni vyema tukakubali kwamba informal money lending business ni illegal, (
ndio maana sishangai kama huyo mama alishinda kesi yake). Sasa ili kucheza na sheria zetu hawa watu wamecreate their own rules (
rules of the jungle actually). Mfano, kama unachukua mkopo wa 2M utasign mkataba kuwa umechukua Mkopo wa 2.4M (
yaan suala la riba halionekani hapo). Kipindi fulani nilikuwa Moshi ndio nilishangazwa, jamaa kapewa mkopo wa 30M (
ambayo ukijumlisha na Riba ya 30% inakuwa 39M) akasainishwa mkataba wa kuuza nyumba kwa 39M (
tarehe inayosomeka ni ile ya marejesho, na wakili anaweka muhuri wake) sasa kama ukidefault nyumba imekwenda.Wale jamaa wa Platnum niliowasema awali wenyewe wanayard kabisa, ukiweka dhamana ya Gari unalipaki hapo, na card unawaachia (
na bado wanawateja wengi tu, the same apply kwa Easy Finance).
Ushauri wangu, ni kuwa ukiingia kwenye biashara hii, fuata zile 5C's zinazohitajika kwenye Microcredit. Ukijua wateja wako vizuri, ukijua tabia zao, ukijua matumizi ya hela wanayoitaka kama itawalipa wao nawe utapata chako, Ukijua uwezo wao, na ukachagua dhamana nzuri utatengeneza faida yako vizuri tena bila kuwa disturbed na regulatory authorities