Jamani nifanyaje kumpata mpenzi mkweli

Jamani nifanyaje kumpata mpenzi mkweli

James strong

New Member
Joined
Aug 19, 2011
Posts
4
Reaction score
1
mpaka sasa nina miaka 35 na sijaoa ingawa natamani sana kufanya,nimedanganywa na wadada wawili,kila mmoja kwa wakati tofauti,sasa naogopa kabisa sasa sijui nifanyaje na kuoa nataka lakini namtafuta mkweli na mwaminifu
 
Wewe ni mwaminifu? Isije ukawa wewe ndio mwenye matatizo......Weka vigezo unavyohitaji nione kama naweza kufit..!
 
wewe mwenyewe ni mkweli kiasi gani??

Wanawake ndio hawa hawa na ukweli wao ndio huo huo.

Angalau tafuta unayempenda, na anayekupenda hata mkidanganyana mtaoneana huruma ya kuumizana mioyo.

Lakini ukikuruputa ukapata muongo kama mie umekwisha.

Mwombe Mungu wako pia akusaidie.
 
Hakuna kama kuingia msikitini na kupiga rakaa zako na ukisha maliza omba dua.

Ramadhan kareem.
 
Hata me nina mawazo kama yako na nimedanganywa kama wewe ni PM labda tutaendana.
 
mpaka sasa nina miaka 35 na sijaoa ingawa natamani sana kufanya,nimedanganywa na wadada wawili,kila mmoja kwa wakati tofauti,sasa naogopa kabisa sasa sijui nifanyaje na kuoa nataka lakini namtafuta mkweli na mwaminifu

Unachotakiwa wewe ni kumtokea demu tu! Unajua, uaminifu sio kitu cha kudumu. Leo aweza kuwa mwaminifu, miaka nane baadae mmoja wenu akaanza kuisaliti ndoa.
 
Safi sana jamaa tena nakupongeza sana kwa kufikia uamuzi uliobora zaidi ktk maisha cha kwanza Muombe MUNGU kwa imani ya dini yako cha pili mtafute binti ambaye moyo wako utalizika nae harafu mweleze. chukua muda kuisoma tabia na mienendo yake pitia topic za JF kuhusu jamaa wanaodanganywa na wachumba wao utapata pa kumuweka mchumba wako namaanisha utajua anakupenda au anakudanganya Cha tatu muonyeshe hali zote za maisha yaanai sio kila akitaka kitu umtimizie sio kila unapokutana nae uwe umechomekea zote hizi utazipata kwenye topic za JF JARIBU kuvuta muda upate kumsoma zaidi kama atakulizisha oa na utukaribishe wana JF japo tuchangie Angalizo [EPUKA KUPENDA KABRA HUJAPENDWA]
 
safi sana, kudanganywa ndio kukomaa kimapenzi, maisha ni milima na mabonde, sasa hujasema tu ulidanganywa vp, walikuwa wake za watu wakakwambia hawajaolewa? au walikudanganya background zao? au walikusaliti? au nini, any way muombe Mungu, pia na wewe usiwe mdanganyifu
 
Mtafute umchunguze wakati ukijichunguza pia. Angalia kiwango chako cha mapenzi siyo yake tu. Kama utakuwa na mapenzi ya kweli utampata mpenzi wa kweli. Pia jitahidi kuepuka papara za vijana wa siku hizi kuanza kutaka vitu vingine ambavyo vinawatia akina dada shaka.
 
Tafakari ni nini kilichokufanya uachane na hao wengine (isije ikawa wewe ni chanzo cha wao kukudanganya). Kama chanzo ni wewe kuwa tayari kujerekebisha. Pia usisahau Kumwomba Mungu akupatie mke mwema.
 
mpaka sasa nina miaka 35 na sijaoa ingawa natamani sana kufanya,nimedanganywa na wadada wawili,kila mmoja kwa wakati tofauti,sasa naogopa kabisa sasa sijui nifanyaje na kuoa nataka lakini namtafuta mkweli na mwaminifu

aah, mbona wapo wengi tu. Sema una bei gani upate mke mkweli na mwaminifu chap chap.
 
Mpenzi wa kweli hana fomula, hapa watu tutakudanganya sana, kinachotakiwa wewe ni kumuomba mungu wako akupatie mke mwema kwa sababu kwake hakuna lisilowezekana
 
Kuna wanaume tumeumbwa na akili ngumu na nzito za kujua nini wanawake wanapenda.
Yaani unakuta mtu kila siku anaharibu na wanawake wanamtosa.
Unaweza kuwa mmoja wao,kaa chini jifunze na urekebishe makosa yako.
 
Miaka 35 ushaanza kuchanganyikiwa?? Watu wana 50 lkn mabachela tu!!
 
Jipe moyo mkuu utafanikiwa tu.. Kikubwa endelea kumuomba MUNGU,nawe uwe mwaminifu utafanikiwa tu.
 
Wamekudangaanya nini? Kuna uongo mwingine ni wa kuupuza tu na kusonga mbele, lakini ukijifanya unatafuta mkweli 100% mkuu utajikuta unagonga 45 huku unaendelea kutafuta.

Kila la kheri mkuu.sema mke ulitakiwa uanze kumtengeneza mapema mkuu, kama 25 hivi,hapo ungekua na mda wa kutosha wa kurekebisha tabia ndogo ndogo kama hizo. Kwa sasa fata ushauri wangu wa kwanza.
 
Back
Top Bottom