Solita
Member
- Nov 29, 2010
- 47
- 4
Mimi ni mdada, nilifanya mtihani wa kidato cha sita mwaka 2007 kama private candidates, baadae nikapata nafasi ya kujiunga na chuo kikuu kwa kutumia cheti changu cha matokeo yaani result slip, shida yangu ni kwamba mpaka sasa sijapat cheti changu cha kidato cha sita kwani kila nikienda necta naambiwa cheti hakionekani, na hata nikiwaambia wanipe utambulisho wowote ili niweze kuomba kazi naambiwa nisubiri kwanza, kusema ukweli hali hii imenifanya nishindwe kuomba kazi yoyote na sijui cha kufanya, naomba ushauri wenu.