Hawa jamaa wameamua kumkomboa mkulima na mfanyabiashara ndogondogo vijijini sasa wanatoa mikopo kwa wakulima sehemu mbalimbali tulioamua kujiingiza kwenye kilimo na hatuna mitaji tuchangamkie hili jamani mi nbimeamua kulima Iringa na wamenikopesha sh lakitatu za kuanzia msimu huu
na kama wangekuwa wana riba kubwa na huduma mbovu wasingekuwa leading microfinace institution in tanzania.jamaa yuko sahihi kuchukua laki 3 na wanatoa hadi mil 50 ukihitaji na kutimiza vigezo.
Riba ya 2.5 kwa mwezi manake ni 30% per year, kama unelima kwa msim mmoja yana 1 year utahitajika kurudisha 390,000 mwisho wa mwaka.
Huo mkopo sio hela kidogo kama ambavo baadhi ya wachangiaji mbavosema, inategemea unataka kuzalisha nini na wapi?
Kwa mfano nipo Karatu,
>Kukodisha Shamba ekari moja 40,000
>Kulima kwa trecta ekari moja 40,000
>Kupanda kwa ng'ombe ekari 1 30,000
>Mbegu za mbaazi ekar moja 14,000
>Kupalilia ekari moja ekar moja 30,000
>Dawa ya wadudu ekari 1 25,000
>Kuvuna ekari moja (VIJANA) 45,000
>Storage 1room 3 months 45,000
TOTAL 269,0000.
Mavuno,
minimum of 6 bags of 100 kgs @ sales at min farm price of 150,000 (nomal market price in arusha ni sh 250,000)
TOTAL REVENUE TZS 900,000
Gross income 631,000
Mvua kama itanyesha kama kawaida mahesabu ndio hayo iyo laki 390, ukitoa unabaki na 241,000 kama una kari kumi then you have a good 2.4mil money. MPO!!!!
Thubutuni VIJANA
Hawa jamaa wameamua kumkomboa mkulima na mfanyabiashara ndogondogo vijijini sasa wanatoa mikopo kwa wakulima sehemu mbalimbali tulioamua kujiingiza kwenye kilimo na hatuna mitaji tuchangamkie hili jamani mi nbimeamua kulima Iringa na wamenikopesha sh lakitatu za kuanzia msimu huu
quotation nzuri, lakini kuna kitu umekisahau. Kuna risk za kutokupata hayo mavuno yanayotarajiwa. Sasa iwapo aliyekopa amekosa mavuno nini kitafuata?
Ndio maana kuna mchangiaji amesema hiyo laki ni bora kukopa kwa ndugu, jamaa na marafiki. Kama benefit yake ni kubwa hivyo sidhani kama ndugu na wengineo watashindwa kumkopesha mwenzao hicho kiasi, hasa ikizingatiwa kwamba tumejenga tamaduni za kuchangiana (ingawa tumeconcentrate zaidi na harusi).
Swali: Je, ni collateral gani wanayoikubali pride kwa mkopo kama huo wa sh. Laki 3?
Heshima kwako Kimpango,
Mkuu wangu laki tatu ni fedha ndogo sana kwenye kilimo kama ni mtu makini unaanza na mkopo wa tshs 5,000,000/= kwenda mbele.Mkuu sijui labda unazungumzia bustani ya nyanya 1/4 eka.Halafu PRIDE wanautaratibu wa marejesho ya wiki kwa mkulima ni ngumu sana mazao mengi yanachukua muda kuanzia miezi miwili hadi sita wakati mwingine hali ya soko inalazimu uweke mazao ghalani hadi bei inapokuwa nzuri sidhani kama PRIDE watavumilia !.