Jamani nimefurahishwa na Pride Tanzania

Jamani nimefurahishwa na Pride Tanzania

kimpango

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2011
Posts
600
Reaction score
717
Hawa jamaa wameamua kumkomboa mkulima na mfanyabiashara ndogondogo vijijini sasa wanatoa mikopo kwa wakulima sehemu mbalimbali tulioamua kujiingiza kwenye kilimo na hatuna mitaji tuchangamkie hili jamani mi nbimeamua kulima Iringa na wamenikopesha sh lakitatu za kuanzia msimu huu
 
Mkuu sijakuelewa, wamekukopesha laki 3? Na vipi riba? Make mikopo ya bongo mziki uko kwenye riba
 
riba yake ni asilimia 2.5 kwa mwezi ila nimependezwa na mikopo ya kilimo marejesho siyo kwa wiki inategemea na zao unalolichukulia na ukuaji wake halafu vigezo vyake ni nafuu
 
Laki tatu unalima vipi mkuu............na kwanini usikope kwa jamaa yako kama mkopo upo hivyo.
 
Subiri maumivu, you will be ripped off by Pride kama huwajui!
 
Huyu muanzisha thread ni kama ana mafanya marketing vile, make mkopo wa laki tatu kwenye kilimo ni utani mkubwa sana na sijui analima kitu gani make hata kilimo cha mchicha kwa hiyo investment ni kiasi kidogo sana.
 
Kwa uzoefu wangu PRIDE ndo wanaoongoza kwa kukubalika,ila tatizo la watanzania huwa tunakurupuka kulaumu kwa kufuata mkumbo bila kujua tatizo. big up PRIDE.
 
Na kama wangekuwa wana riba kubwa na huduma mbovu wasingekuwa Leading Microfinace Institution in Tanzania.Jamaa yuko sahihi kuchukua laki 3 na wanatoa hadi mil 50 ukihitaji na kutimiza vigezo.
 
Sasa mtu unamkopesha laki tatu unataka akalime nini kama sio kumuongezea misalaba ya maisha.............jitahidini kuwakomboa watu wenye kipato kidogo sio kuwafanya mateja wa PRIDE kutwa wapo huko.
 
Hawa jamaa wameamua kumkomboa mkulima na mfanyabiashara ndogondogo vijijini sasa wanatoa mikopo kwa wakulima sehemu mbalimbali tulioamua kujiingiza kwenye kilimo na hatuna mitaji tuchangamkie hili jamani mi nbimeamua kulima Iringa na wamenikopesha sh lakitatu za kuanzia msimu huu

Uzi ungekuwa mtamu kama ungetoa na kamchanganuo kidogo, jinsi utakavyoitumia hiyo laki tatu kulimia huko Iringa. Unaweza ukawa unataka kulima eka moja ya mahindi,shamba ni lako, nguvu kazi ni wewe mwenyewe na mbegu unaomba kwa mjomba, labda hiyo laki tatu ni mbolea na palizi.

Hebu toa maelezo tukuelewe,namna gani utatumia hiyo laki tatu.
 
Mi naomba mnisaide hii hesabu. Asilimia 2.5 kwa mwezi ni sawa na asilimia ngapi kwa mwaka ili tujue hiyo interest rate ni kiasi gani kwa mwaka ili tuone wako poa au vipi. Strategies nyingine bwana........
 
na kama wangekuwa wana riba kubwa na huduma mbovu wasingekuwa leading microfinace institution in tanzania.jamaa yuko sahihi kuchukua laki 3 na wanatoa hadi mil 50 ukihitaji na kutimiza vigezo.

mkuu hakuna cha kuongoza wala nini, hao wote wako katika kuwanyonya wateja wao na wanahakikisha unakua mteja wao wakudumu, hizo riba zao bado ni kubwa sema mtu akiambiwa arudishe kwa mwezi anaona ni kidogo sana.
 
Nakupa pole we uliyekopa laki tatu Pride, hili ni shirika linaloongoza kwa kuwapa umasikini watanzania popote pale lilipo ni hatari sana. Tatizo ni katika utozaji wa riba, kwanza riba ni kubwa pili wanatumia fomula ya flat riba yaani wanapigia hesabu ya riba ya mwaka mzima haijarishi unalipa kila mwezi, kama umekopa ml 5 basi wanataka riba ya mwaka mzima na papo hapo unaambiwa kila mwezi urejeshe. Je huo si wizi? Watanzania tuzinduke tutakamuliwa mpaka lini?
 
Riba ya 2.5 kwa mwezi manake ni 30% per year, kama unelima kwa msim mmoja yana 1 year utahitajika kurudisha 390,000 mwisho wa mwaka.
Huo mkopo sio hela kidogo kama ambavo baadhi ya wachangiaji mbavosema, inategemea unataka kuzalisha nini na wapi?
Kwa mfano nipo Karatu,
>Kukodisha Shamba ekari moja 40,000
>Kulima kwa trecta ekari moja 40,000
>Kupanda kwa ng'ombe ekari 1 30,000
>Mbegu za mbaazi ekar moja 14,000
>Kupalilia ekari moja ekar moja 30,000
>Dawa ya wadudu ekari 1 25,000
>Kuvuna ekari moja (VIJANA) 45,000
>Storage 1room 3 months 45,000

TOTAL 269,0000.

Mavuno,
minimum of 6 bags of 100 kgs @ sales at min farm price of 150,000 (nomal market price in arusha ni sh 250,000)
TOTAL REVENUE TZS 900,000
Gross income 631,000
Mvua kama itanyesha kama kawaida mahesabu ndio hayo iyo laki 390, ukitoa unabaki na 241,000 kama una kari kumi then you have a good 2.4mil money. MPO!!!!
Thubutuni VIJANA
 
Quotation nzuri, lakini kuna kitu umekisahau. Kuna risk za kutokupata hayo mavuno yanayotarajiwa. Sasa iwapo aliyekopa amekosa mavuno nini kitafuata?
Ndio maana kuna mchangiaji amesema hiyo laki ni bora kukopa kwa ndugu, jamaa na marafiki. Kama benefit yake ni kubwa hivyo sidhani kama ndugu na wengineo watashindwa kumkopesha mwenzao hicho kiasi, hasa ikizingatiwa kwamba tumejenga tamaduni za kuchangiana (ingawa tumeconcentrate zaidi na harusi).

Swali: Je, ni collateral gani wanayoikubali PRIDE kwa mkopo kama huo wa sh. laki 3?
 
Heshima kwako Kimpango,

Mkuu wangu laki tatu ni fedha ndogo sana kwenye kilimo kama ni mtu makini unaanza na mkopo wa tshs 5,000,000/= kwenda mbele.Mkuu sijui labda unazungumzia bustani ya nyanya 1/4 eka.Halafu PRIDE wanautaratibu wa marejesho ya wiki kwa mkulima ni ngumu sana mazao mengi yanachukua muda kuanzia miezi miwili hadi sita wakati mwingine hali ya soko inalazimu uweke mazao ghalani hadi bei inapokuwa nzuri sidhani kama PRIDE watavumilia !.

Hawa jamaa wameamua kumkomboa mkulima na mfanyabiashara ndogondogo vijijini sasa wanatoa mikopo kwa wakulima sehemu mbalimbali tulioamua kujiingiza kwenye kilimo na hatuna mitaji tuchangamkie hili jamani mi nbimeamua kulima Iringa na wamenikopesha sh lakitatu za kuanzia msimu huu
 
quotation nzuri, lakini kuna kitu umekisahau. Kuna risk za kutokupata hayo mavuno yanayotarajiwa. Sasa iwapo aliyekopa amekosa mavuno nini kitafuata?
Ndio maana kuna mchangiaji amesema hiyo laki ni bora kukopa kwa ndugu, jamaa na marafiki. Kama benefit yake ni kubwa hivyo sidhani kama ndugu na wengineo watashindwa kumkopesha mwenzao hicho kiasi, hasa ikizingatiwa kwamba tumejenga tamaduni za kuchangiana (ingawa tumeconcentrate zaidi na harusi).

Swali: Je, ni collateral gani wanayoikubali pride kwa mkopo kama huo wa sh. Laki 3?

jembe halimtupi mkulima wahenga walisema, biashara zote zina matatizo yake!
 
Heshima kwako Kimpango,

Mkuu wangu laki tatu ni fedha ndogo sana kwenye kilimo kama ni mtu makini unaanza na mkopo wa tshs 5,000,000/= kwenda mbele.Mkuu sijui labda unazungumzia bustani ya nyanya 1/4 eka.Halafu PRIDE wanautaratibu wa marejesho ya wiki kwa mkulima ni ngumu sana mazao mengi yanachukua muda kuanzia miezi miwili hadi sita wakati mwingine hali ya soko inalazimu uweke mazao ghalani hadi bei inapokuwa nzuri sidhani kama PRIDE watavumilia !.

ngoja kidogo, umewahi pitia jamaa wanaitwa PASS wao wanatoa mikopo mikubwa zaidi ya milion5, but you should have a viable business plan.
 
Back
Top Bottom