PROF. ENG
Senior Member
- Nov 15, 2011
- 122
- 35
Mi ni mume wa mtu na watoto wawili. Kuna mdada ni mke wa mtu na ana mtoto mmoja. Karibu miaka miwili sasa huyu mdada kuna kazi za kiofisi tumekuwa tukishirikiana. yeye yupo kampuni nyingine. Tumekuwa tukikutana kwenye vikao mara kwa mara. Tangu tuanze kukutana naona ukaribu unazidi kuwa mkubwa baina yetu wawili, na mi nahisi kumkumbuka mara kwa mara, na yeye pia nahisi ni kama hivyo, sababu wakati mwingine napata salamu za mara kwa mara bila kutegemea kutoka kwake. Mimi ni mume wa mtu na naheshimu sana ndoa na familia yangu na sijawahi kucheat tangu nifunde ndoa miiaka 7 iliyopita. Lakini nahisi kuingia kwenye mtego hivi hivi najiona na wakati mwingine roho inanisuta inaniambia hapana usifanye hivyo utakuwa umetenda kosa kubwa sana. Mbaya zaidi kila tunapokutana na huyu mdada najihisi kuwa karibu naye kupita kiasi, na yeye pia, na nahisi kuvutiwa naye sana, baadhi ya watu ofisini wameshatambua hilo. Jamani hivi nimerogwa au!!!, maana tukishaachana naanza kujuta kuwa karibu naye namna hiyo.