Haitajiki elimu ya phd kumfaham JUHA!!
Watu mnshindwa kuelewa kuwa mapenzi yapo.. Na kuoa hakumaanishi kushindwa kupenda tena!
Wengi wetu ni mashahidi wa ndoa nyingi zinazofungwa na huku wanandoa hao wakiwa wameacha wapenzi wao,kutokana na kushindwa tu kuoana,na si kushindwa kupendana.
Ila kwa mtoa mada,najua unayoyapitia.. Sijui ndoa yako ikoje,lakini chanzo kingine cha moyo kupenda mtu mpya,ni migogoro au mgogoro sugu kwenye ndoa. Hata kama hakuna mgogoro lakini wataalamu wanashauri "kuirenew" ndoa,kwa vitu tofauti.
Mkishakuwa na watoto,ndiyo ndoa hupooza maana mnawaza mambo ya kifamilia wala mambo yenu wawili kama mke na mume hamyafanyi! Hamtoki out,beach,dinner,utani hakuna tena,na vitu kama hivyo...
Ukinisoma vizuri utanielewa,ila si dhambi,ila ni hali halisi na wewe si wa kwanza kutokewa na hali hiyo.
Kuna wengine wanalaumu,dharau,tusi,wakati hata kama hujavua nguo na kucheat,unapomuangalia kwa kumtamani ni sawa na kuzini naye tayari!
Unamwangalia na kumtofautishaje mtu anayetaabika na ndoa yake,na kukosa mapenzi na mwenza wake,lakini anakutana na mtu anayemjali kwa jambo dogo,wakatokea kuelewana na yule anayekondeana kwa kutaabika na ndoa yake,lakini,aidha amekosa wa kumliwaza,au kukwepa kuzini kama anavyoshauriwa mwenzetu na wengine humu ndani..