Jamani nimelogwa au!!!!!

PROF. ENG

Senior Member
Joined
Nov 15, 2011
Posts
122
Reaction score
35
Mi ni mume wa mtu na watoto wawili. Kuna mdada ni mke wa mtu na ana mtoto mmoja. Karibu miaka miwili sasa huyu mdada kuna kazi za kiofisi tumekuwa tukishirikiana. yeye yupo kampuni nyingine. Tumekuwa tukikutana kwenye vikao mara kwa mara. Tangu tuanze kukutana naona ukaribu unazidi kuwa mkubwa baina yetu wawili, na mi nahisi kumkumbuka mara kwa mara, na yeye pia nahisi ni kama hivyo, sababu wakati mwingine napata salamu za mara kwa mara bila kutegemea kutoka kwake. Mimi ni mume wa mtu na naheshimu sana ndoa na familia yangu na sijawahi kucheat tangu nifunde ndoa miiaka 7 iliyopita. Lakini nahisi kuingia kwenye mtego hivi hivi najiona na wakati mwingine roho inanisuta inaniambia hapana usifanye hivyo utakuwa umetenda kosa kubwa sana. Mbaya zaidi kila tunapokutana na huyu mdada najihisi kuwa karibu naye kupita kiasi, na yeye pia, na nahisi kuvutiwa naye sana, baadhi ya watu ofisini wameshatambua hilo. Jamani hivi nimerogwa au!!!, maana tukishaachana naanza kujuta kuwa karibu naye namna hiyo.
 
onja uone kama huchongi mzika,
ushauri wa bure, run ...run .... away for you marriage... ukijaribu tu , utamsahau mkeo maana vimada wanakuwaga na juhudi vibaya sana
 
Unaonekana ushatamani mkuu! Kula fasta, osha mikono na omo, sugua mdomo kwenye mchanga kama mmbwa mwitu, then sepa fastaa sanaaa.
 
Kaka mkubwa cyo kulogwa, hvyo vi2 humtokea kila m2. Kumpenda mkeo ni kuchagua kuwa comited kwake na kumuheshimu kwenye nyakati kama hizi ambazo feelings ziko kwa mwingine(actualy, that is the true meaning of love)
 
Sema unataka Kucheat, maana Mtu ambaye anapenda Ndoa yake na hapendi kuvunja Agano huwa anajiepusha na Vitu kama hivyo..

Ukifikiria sana kuhusu Yeye ndo utazidi kuvutwa nae. Acha kumfikiria na Weka mawazo yako kwenye Ndoa yako.
 
unajua thats very natural ukiwa karibu ujenga mazoea na mwiaho unagundua mazuri ya huyo mtu na kudhani unampenda
wewe chukufanya ni kupunguza ukaribu mliokuwa nao na kujikumbusha kuwa ndoa yako ndio muhimu
 
duh, hadi hapa ushakwenda na maji weye.
Naona timu pinzani inaongoza 3-0

pole, panga safu yako ya ulinzi vizuri, kama wa kusali sali sana, kaa naye mbali, jisogeze karibu na mkeo zaidi.
 
Kama unamapenzi mema na wanao na mkeo achana nae haraka,mwisho wa siku namkeo ataachana nawewe,utatakiwa kulea watoto mwenyewe na kuwanyima haki yao ya kimsingi, itakayo pelekea watoto kukosa malezi ya pande mbili matokeo yake watoto kuwa malaya na kuvuta bangi.USITHUBUTU KWA AFYA YAKO NA FAMILIA YAKO!
 
Tatizo siku zote ni kutojitambuwa lakini wewe si umeshajitambuwa? Amuwa unataka kulamba au hutaki basi. Roho unavyoielekeza ni rahisi kukubaliana nawe!
 
Ana nini ambacho mkeo hana.........?

hata sijui ndugu. Ni vile tu tukikuatana tunakuwa karibu sana kupita kiasi bila mi mwenyewe kujitambua. Kiasi kwamba hata wenzangu wameshahisi kuwa nimeshatekwa. Kumkimbia inakuwa kazi sababu tunashirikiana kazi za kiofisi. Na baadhi ya watu wameshaanza kuhisi nimeshaua.
 
Usitafute mchawi sehemu nyinge. Unaye hapo hapo. Naye ni TAMAA YA MWILI. Mkemee kwa jina la Yesu ataondoka mara moja.
 
muhadithie mkeo,,

Hapo nitazua balaa mkuu. Kazi hazitafanyika. Ila kwa namna moja au nyingine anamfahamu kwasababu ya mawasiliano ya kiofisi ambayo tunayo. Hizo ishu zingine wife hajui na itakuwa balaa zaidi akijua. sithubutu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…