Jamani nimenunua kuku

Jamani nimenunua kuku

swissme

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2013
Posts
13,663
Reaction score
19,894
Naombe mnielekeze jinsi ya kumtengeneza pls kukaanga au kulost au aina yoyote.mate yanatoka
 
Kama ni kuku mzima fanya hivi:
Mkate vipandepande muwekee kitunguu saumu kijiko kimoja cha supu kilichotwangwa,pilipili manga nusu kijiko cha chai,chumvi,ndimu.Muache masaa kadhaa viungo vikolee.Kisha mkaange.

Ukitaka kumroast muweke viungo hivo nilivyotaja juu pamoja na tangawizi kidogo kama kijiko cha chai kimoja.kisha mchemshe na maji kidogo kwanza ili viungo vikolee,kisha muongeze maji aive.
Mahitaji ya roast
kitunguu 1
nyanya 5
carrot 2 zimenye,na uisugue kwenye chombo cha kusugulia carrot iwe hivi
Viazi vitano
carrot.jpg
pilipili hoho 1/2
kitunguu saumu kijiko kimoja cha chai
chumvi
mafuta ya kukaangia
nyanya ya kibati

  • Kaanga kitunguu kimoja kikubwa,kilichokatwa vipandepande kikianza kubadilika rangi weka hizo karoti,zikaange nazo mpaka zibadilike rangi
  • Weka viazi na nyanya,nyanya ya kibati pamoja na viungo unavyopendelea
  • Nyanya zikilainika weka supu ya kuku na kuku
  • Weka pilipili hoho ilokatwa vipande
  • Uache uchemke mpaka uwe mdikodiko,kisha epua kwakuliwa
 
Nimerudi kusema Asanten sana wote hapo juu laki gorgeousmimi nimekukubali karibu next chicken.
 
Back
Top Bottom