Jamani, nimeokota mapesa!

Kwa nabii flora kulikuwa na shuhuda motomoto za waumini kuokota mamilioni kwenye daladala, kwenye magodolo n.k
Lakini next Sunday yule muumini sadaka anatoa buku na kuonyesha ishara kuwa asubuhi hajapata chai.
Yes.
Yesu yupo anaweza kutumia malaika kugawa pesa n.k
Mungu akubariki
 
tangazo limekaa kimkakati ukizingatia valentine iko jirani utakuwa na kazi kubwa uko pm.
 
Hongera..!! Kuna Uwezakano Kama Ikikuwia Vyema Ukaniwezesha Shilingi 10000 Ya Kitanzania?
Usimuombe mtu pesa. Muombe Mungu. Fedha na dhahabu ni mali yake.
Hii ni ahadi ya Yesu kwamba tukimuomba Mungu tutapewa. Mathayo 7:7-12
“Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa kuwa kila aombaye hupewa; naye kila atafutaye hupata; na kila abishaye hufunguliwa mlango. “Au ni nani miongoni mwenu ambaye mwanawe akimwomba mkate atampa jiwe? Au mwanawe akimwomba samaki atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?..."
 
ikiwa ni mwaminifu,mcha Mungu,bora apeleke polisi kama mali ya kuokota,kisha apewe RB itakayomfanya akae kwa kipindi fulani,asipopatikana mwenyewe ndipo atapewa kutumia kama pesa za kuokota zilizokosa mwenyewe.
Imeandikwa wapi hiyo, maana tunaongozwa na Maandiko Matakatifu
 
tangazo limekaa kimkakati ukizingatia valentine iko jirani utakuwa na kazi kubwa uko pm.
Sio tangazo, ni habari. Hata hivyo, upendo unapaswa kuonekana siku zote, siyo Valentine Day tu. Waebrania 13:1-8 "Upendano wa ndugu na udumu..."
 
Be blessed
 
sheria za nchi zinasema hivyo.
Hahaa. Nchi ipi, na mimi niko nchi ipi? In every corner of this world, kila nchi ina sheria zake. We're all living under different rules—each country brings its own flavor, its own way of governing life. So, remember: no matter where you are, each nation stands unique with its own set of laws and customs. Tuko pamoja?
 
Katika sheria ya Uislamu, mali ya kuokota, ikiwa ina thamani kubwa basi inabidi uitangaze kwa muda wa mwaka mmoja.

Baada ya hapo ikiwa hajapatikana mwenyenayo ndio inakuwa halali yako, unaweza kuitumia.
 
Haya!!Uwe Na Siku Njema
 
Lengo la uzi umelielewa ila sema umebaki na maswali. Halafu ungejuaje mimi ni mwaminifu kama nisingesema? Hata Yesu alijitaja jinsi alivyo: "Mimi ni Nuru ya Ulimwengu... Mimi ni Njia na Kweli na Uzima. .. Mimi ni Mchungaji Mwema nk nk." Hivyo usishangae kusikia ninajiita "Mwaminifu" Ndivyo nilivyo, ni tabia yangu.
 
Yesu alishawahi kusema yeye ni mwaminifu
 
Na mitego ya Shetani huwa inapitia kwenye shida ulizonazo.
Sidhani kama M-ungu analeta riziki kwa njia ya kuokota bali baraka za kazi uzitendazo.
Shetani haniwezi mimi. Nimepewa mamlaka ya kumkemea kwa Jina la Yesu.
Nimekuambia unaweza kufanya kazi usipate pesa/wateja. Hivyo usiweke matumaini yako yote kwenye kazi yako. By the way, hujasoma habari za wana wa Israeli jangwani? Soma 📖 Kutoka 16:14-15. Kila siku walikuwa wanaokota "mana"(chakula kitamu sana). Unashangaa mimi kuokota mapesa kwa siku moja tu? Je, ningekuambia kila siku naokota?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…