Jamani, nimeokota mapesa!

Ubarikiwe sana mtumishi. Kweli kila asemaye Mungu hayupo ni mpumbavu
 
Lete tupicha picha
 
Mimi nikitoa sadaka, sipigi tarumbeta🎺kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. Mt 6:2
 
Mimi nikitoa sadaka, sipigi tarumbeta🎺kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. Mt 6:2
ni muhimu zaidi sifa na utukufu wa Mungu kwenye maisha yetu, vikaambatana na ushuhuda wa shukrani madhabahuni, kuliko kujisifu kwa wema mitandaoni
 
Niumie Fungu la Kumi nikubariki uendelee kupokea miujiza.
 
shukrani madhabahuni,
Kumbuka kisa cha wale wenye ukoma kumi. Baada ya kutendewa muujiza wa uponyaji, waliambiwa wakajionyeshe kwa makuhani, sio wakatoe sadaka ya shukrani kwa makuhani. Katika wale kumi mmoja tu ndiye aliyetambua shukrani anapaswa kupewa Yesu, akarudi kutoa shukrani kwa Yesu, na Yesu akamsifia.
Lk 17:11-18
Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, alikuwa akipita katikati ya Samaria na Galilaya. Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali, wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu! Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika. Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu; akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria. Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu?

Yesu ni Mungu. Yupo mahali pote. Shukrani zinazotolewa hata kwa njia ya mitandao anaziona na anazipokea.
 
Niumie Fungu la Kumi nikubariki uendelee kupokea miujiza.
Mtu habarikiwi kwa kutoa fungu la kumi tu bali kwa kusikia na kutenda kila neno aliloliagiza Mungu. Soma uzi huu ujue vigezo na masharti ya kubarikiwa
 
napendekeza sifa, utukufu na shukrani zielekezwe kwa Mungu muweza wa yote,

na sio kujisifia wenyewe binafsi ya kwamba tu watu wema mitandaoni, baada ya neema na baraka za Mungu kutamalaki katika maisha yetu. Tumrudishie Mungu shukrani hadharani
 
na sio kujisifia wenyewe binafsi ya kwamba tu watu wema mitandaoni
Mkuu, soma vizuri uzi wangu. Mwishoni nimesema hivi: "Jamani Mungu ni Mkuu sana! Nawasikitikia wanaosema eti Mungu hayupo. Wanakosa baraka nyingi. Tangu nimwamini Yesu, nimeona miujiza mingi ya kupita kawaida. Hata huo ni muujiza. Nilikuwa na shida ya pesa, nikamuomba Mungu, amenipa mapesaaa!"

Hayo maneno yananisifu mimi au yanamsifu Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…