maiko sultan
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 549
- 1,492
Weka picha ya hayo mapesa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ikiwa ni mwaminifu,mcha Mungu,bora apeleke polisi kama mali ya kuokota,kisha apewe RB itakayomfanya akae kwa kipindi fulani,asipopatikana mwenyewe ndipo atapewa kutumia kama pesa za kuokota zilizokosa mwenyewe.YEsu yupo naye
Hakunaga hiyooikiwa ni mwaminifu,mcha Mungu,bora apeleke polisi kama mali ya kuokota,kisha apewe RB itakayomfanya akae kwa kipindi fulani,asipopatikana mwenyewe ndipo atapewa kutumia kama pesa za kuokota zilizokosa mwenyewe.
Umeandika ukiwa na wenge jingi sana halafu umejichanganya hata haueleweki, lengo la huu uzi ni nini?Heshima zenu Wakuu! Nawaletea habari ya kweli, kweli kabisa, maana mimi nauchukia uongo kama ukoma! Nimeokota mapesa. Sasa usiniulize ni dola ngapi, usije ukashawishika kunifuata uninyang’anye!
Wewe jua tu nimeokota mapesa kama wana wa Israeli walivyookota “mana” jangwani. Mimi nafanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato.
Hata hivyo, pamoja na kufanya kazi ninamtegemea Mungu kila wakati, kwakuwa najua unaweza kufanya biashara usipate wateja/pesa. Unaweza kuajiriwa ukafukuzwa kazi.
Unaweza kupata pesa zikaibiwa zote! Hivyo ni muhimu kumtegemea Mungu. Kwa kufanya hivyo nimeona Mungu akinifanikisha na kunitendea miujiza mingi.
Haya, turudi kwenye mada. Ilikuwa hivi: Kuna watu watatu walikuja ofisini kwangu wiki iliyopita, kwa wakati tofauti na siku tofauti. Wote ninawafahamu na huwa ninawasiliana nao.
Niliwahudumia wakaondoka. Jana mchana, niliingia ofisini kwangu, nikachungulia chini ya viti vya wageni. Kwa mshangao mkubwa nikaona mapesa! Mimi ni mwaminifu sana kwa habari ya pesa.
Nikija dukani kwako ukinizidishia chenji nakurudishia. Nikasema moyoni mwangu haya mapesa nadhani ni wale jamaa waliokuja ofisini kwangu wameyadondosha. Siwezi kuyatumia.
Nikawapigia simu na kuwauliza kama waliona upungufu wa pesa kwenye mifuko yao baada ya kuondoka. Wote wakakataa na kunipa kibali cha kuyatumia hayo mapesa.
Jamani Mungu ni Mkuu sana! Nawasikitikia wanaosema eti Mungu hayupo. Wanakosa baraka nyingi.
Tangu nimwamini Yesu, nimeona miujiza mingi ya kupita kawaida.
Hata huo ni muujiza. Nilikuwa na shida ya pesa, nikamuomba Mungu, amenipa mapesaaa! Stay blessed!
Mungu yupo tu hata nisingeokota. Point yangu ni kwamba nilikuwa na shida ya pesa, nikamuomba Mungu akanipa mapesa kwa njia hiyo ya muujiza. Huo ni udhihirisho kuwa Mungu yupo, anasikia maombi yetu na kutupatia haja zetu.Kwa kuokota pesa ndio mungu yupo🤣😂, kwahiyo usingeokota!? 😂🤣
...hayupo!Kwa kuokota pesa ndio mungu yupo🤣😂, kwahiyo usingeokota!? 😂🤣
Yaani awapelekee polisi? Ni za kwao?Mkuu,hizo pesa zitakuletea shida acha ujuaji,kama unamwogopa Mungu,Kalipoti polisi,ipo siku waliozisahau hizo pesa watakumbuka na kuja tena ofsini kukudai!
Sasa hatuelew mna mwamini Nan kama n yesu ama laahHakunaga hiyoo
huo ndio ucha MUNGU?Hakunaga hiyoo
Ariiiiiiiiiise!Heshima zenu Wakuu! Nawaletea habari ya kweli, kweli kabisa, maana mimi nauchukia uongo kama ukoma! Nimeokota mapesa. Sasa usiniulize ni dola ngapi, usije ukashawishika kunifuata uninyang’anye!
Wewe jua tu nimeokota mapesa kama wana wa Israeli walivyookota “mana” jangwani. Mimi nafanya kazi kwa bidii ili kujipatia kipato.
Hata hivyo, pamoja na kufanya kazi ninamtegemea Mungu kila wakati, kwakuwa najua unaweza kufanya biashara usipate wateja/pesa. Unaweza kuajiriwa ukafukuzwa kazi.
Unaweza kupata pesa zikaibiwa zote! Hivyo ni muhimu kumtegemea Mungu. Kwa kufanya hivyo nimeona Mungu akinifanikisha na kunitendea miujiza mingi.
Haya, turudi kwenye mada. Ilikuwa hivi: Kuna watu watatu walikuja ofisini kwangu wiki iliyopita, kwa wakati tofauti na siku tofauti. Wote ninawafahamu na huwa ninawasiliana nao.
Niliwahudumia wakaondoka. Jana mchana, niliingia ofisini kwangu, nikachungulia chini ya viti vya wageni. Kwa mshangao mkubwa nikaona mapesa! Mimi ni mwaminifu sana kwa habari ya pesa.
Nikija dukani kwako ukinizidishia chenji nakurudishia. Nikasema moyoni mwangu haya mapesa nadhani ni wale jamaa waliokuja ofisini kwangu wameyadondosha. Siwezi kuyatumia.
Nikawapigia simu na kuwauliza kama waliona upungufu wa pesa kwenye mifuko yao baada ya kuondoka. Wote wakakataa na kunipa kibali cha kuyatumia hayo mapesa.
Jamani Mungu ni Mkuu sana! Nawasikitikia wanaosema eti Mungu hayupo. Wanakosa baraka nyingi.
Tangu nimwamini Yesu, nimeona miujiza mingi ya kupita kawaida.
Hata huo ni muujiza. Nilikuwa na shida ya pesa, nikamuomba Mungu, amenipa mapesaaa! Stay blessed!
wakikuambia kuwa ni kiasi kikubwa cha pesa tofauti na ulizoyikuta humo utaweza kulipa? Think twice.No worries! Waliozisahau wakija kunidai nawarudishia mapesa yao😀