Jamani nisaidieni kazi yoyote!!!

Okay, usijali hata kama hiyo one hour imeshapita na uko offline kwa sasa. Ukirudi online angalia katika PM, kuna job post nimeiona mahali na nimekuwekea huko.

asante sana kwa kunitumia hiyo post.nashukuru nitaifanyia kazi.
 
Bint

NiPM CV yako ukiambatanisha na picha kuna jamaa najuana nao ofisi ya mipango pale!

asante nitakutumia CV ila picha sitaweza ndugu yangu kama kunisaidia mpaka nitume picha nisamehe.
 
sante ndugu yangu kwa ufafanuzi.
kwa kifupi karibia kila kozi tuna soma mpaka account,bussiness law,information technology vyote tunasoma kwa hiyo naweza kazi aina hizo
 
asante nitakutumia CV ila picha sitaweza ndugu yangu kama kunisaidia mpaka nitume picha nisamehe.
sina uhakika na malengo ya mkuu masalino lakini ni kweli sehemu nyingi siku hizi wanahitaji picha na hasa serikalini...
 
Bint

NiPM CV yako ukiambatanisha na picha kuna jamaa najuana nao ofisi ya mipango pale!
mkuu ili kumtoa wasiwasi aende akawaone moja kwa moja na hiyo picha yake baada ya kumpm hizo contacts
 
Pole ila usikate tamaa hapa umefika la msingi usichukulie sana hili jambo too personal kutafuta kibarua ni changamoto tuu, ni pm na mimi CV yako nitaituma sehemu tofauti.
 
Pole ila usikate tamaa hapa umefika la msingi usichukulie sana hili jambo too personal kutafuta kibarua ni changamoto tuu, ni pm na mimi CV yako nitaituma sehemu tofauti.
 
asante sana kwa kunitumia hiyo post.nashukuru nitaifanyia kazi.

Sary,
Huyo ndiyo Masanilo. Utani mwiingi saana. Kama hujawazowea Wasukuma basi ndiyo inabidi uanze. Ila na utani wake wote nina imani kuwa anaweza kuwa mtu atakayekusaidia. Waweza kutuma CV bila bicha na hata kama ukituma picha so what? Yeye yuko huko Kyela na wewe Dodoma. Pia hana anwani yako ya nyumbani kwahiyo hata akitaka kukutana na wewe basi itakuwa ni uamuzi wako mwenyewe. Tusiwe watu wa kuogopa namna hiyo maana mtu anaweza kuwa kauliza kwa lengo zuri. Jamani dunia ya leo kama mtu anakutafuta kwa lengo lolote lile ni rahisi sana kukupata. Kwani akikupa anwani uende kwa rafiki yake na rafiki yake achukue data zako zote si bado atakupata tu popote pale ulipo?
Ukitaka usipatikane dunia ya leo basi usiwe ONLINE......

Umefanya vizuri kuleta swala lako hapa maana wanasema "mgaagaa na upwa, hali wali mkavu". Mungu akusaidie katika hilo ili ufanikiwe kwani una malengo mazuri (kama mtoto wa kwanza) ili uweze saidia mdogo wako na nduguzo.
 
vp umepata tayari au bado.....tafadhari tupe updates.....
''mvumilivu hula mbivu.........ila mvundika mbivu hula mbovu''
 
Masa si ungesema tu akutumie picha yake mchezo uishe!! Hata mimi naitamani sijui ataniPm.

siyo anataka picha yake, siku hizi ofisi nyingi za serikali ukituma application wanataka na passport size, ili siku ya interview asije mtu mwingine
 
vp umepata tayari au bado.....tafadhari tupe updates.....
''mvumilivu hula mbivu.........ila mvundika mbivu hula mbovu''

sijapata jamani ndo jana tu nimeomba kwenu.nikifanikiwa nitawambia ila bado ndo nafanyia kazi ile niliyotumiwa na sinkala.

kama ipo nisaidie jamani.
 
Pole ila usikate tamaa hapa umefika la msingi usichukulie sana hili jambo too personal kutafuta kibarua ni changamoto tuu, ni pm na mimi CV yako nitaituma sehemu tofauti.

asante nitalifanyia kazi
 
asante nitakutumia CV ila picha sitaweza ndugu yangu kama kunisaidia mpaka nitume picha nisamehe.

safi sana,
mwambie HUDANGANYIKIIIIIII!,

ala.
 
Kazi nimeweka nyingi za Tanzania hapa myafricancareer.blogspot.com
 
asante nitakutumia CV ila picha sitaweza ndugu yangu kama kunisaidia mpaka nitume picha nisamehe.

Ur wrong!

safi sana,
mwambie HUDANGANYIKIIIIIII!,

ala.

Unaishi dunia gani wewe!

siyo anataka picha yake, siku hizi ofisi nyingi za serikali ukituma application wanataka na passport size, ili siku ya interview asije mtu mwingine

Joyceline

Umekuwa mkweli, sihitaji picha yake yeye kama yeye, kuna ufisadi sana siku hizi hasa kwenye secta ya ajira, unakuta anayeandika barua ya kuomba kazi ni Sikonge siku ya Interview anazuka Engineer! Hata vyuo vikuu siku hizi lazima uambatanishe na passport size zako ilikuepusha wengine kusomea vyeti vya wengine.

Jamani demu wa kwenye mtandao unaweza kuinvest mimi huchukulia kama ni scam tu, suppose akituma picha ya pretty ama Joyceline ndo nianze kumwaga sera ? watu wanaufinyu wa mawazo sana hapa. Sary umenidassapoint sana nadhani hata hiyo kazi niliyokupigia chepeto hutaiweza maana uwezo wako wa kufikiri nina mashaka nao sana.

All the best on your job search

Mzee Masa - Kyela
 
Acha hasira kaka,
kumbuka ni sisi sisi hapa kila siku tunasema wasichana wa siku hizi maharage ya mbeya, ooh, wako easy, so watu wanajitahidi kuwa waangalifu na pia hawawezi kujua lengo lako unless umemwelewesha vizuri na kuwa wazi ili ajue anachofanya, hata ningekuwa mimi kwenye nafasi yake may be i would have done the same, may be. lakini ulichokuwa unatakiwa kufanya masanilo ni kumwelewesha tu kama walivyofanya watu hapa na ninatumaini angefanya ulivyomwagiza. please msaidie tu, usikasirike wala kumsusa.
Japo simjui lakini i feel she is in need and i understand the stress she is in maana kutafuta kazi si mchezo, na inawezekana huko alikopita kakutana na mambo ya kutakiwa atoe ngono ndo apate kazi mara nyingi tu ndo maana yuko alert hivyo.
Ukiwa kama mwelewa masanilo elewa stress aliyo nayo na umsaidie tu kwa moyo, na Mungu atakuona ulchofanya, wanasema tenda wema uende zako...........
 
Ndugu zanguni ninafuraha kuwapata taarifa kuwa nimefanikiwa kupata kazi katika manisipaa moja nchini kama Afisa maendeleo ya mji.Hivyo wote mliojitokeza na kunitia moyo kweli nashukuru sana.Pia nashukuru kwa michango yenu mizuri milokuwa mnachangia ili kuhakikisha kilio changu kinatatuliwa.

Kwa kweli ni furaha isiyo nakifani.
Pia napenda kuchukuwa nafasi hii pia kumuomba msamaha ndugu yangu masanilo kwa kumkwaza na kumdisaapoint kwa jibu nililompa la kutomtumia picha.Kwa kweli sikujua kama siku hizi kama kuna watu wanafanya uhuni wa namna hiyo kwamba mtu anaitwa John kwenye interview halafu anaenda Abdallah.Lakini kwa kifupi hakuna kilichoharabika kikubwa nawatakia kazi njema na moyo kama huu mliouonyesha kwangu uendelee hata kwa watu wengine.

Mungu ibariki Tanzania mungu ibariki JF na wanachama wake wote kuanzia ngazi ya member mpaka ya JF expert member.

Yours
Sarah
 
Masanilo poleeeeeee!!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…