Jamani Tatizo ni nini hasa?

Jamani Tatizo ni nini hasa?

Salama iko wana JF?

Nina jambo kidogo linanitatiza katika karne hii ya utandawazi..

Kuna hii issue ya mahusiano yaliyopo sasa....
Ukijaribu kuuliza mabinti issue ya kuoa na kuolewa utasikia majibu yao waoaji hawapo siku hizi
Ukiuliza wanaume nao jibu utasikia ni lile lile siku hizi waolewaji hawapo
Inakuwaje wakati idadi ya single wakike na single wa kiume ni wengi sana
Kwanini jibu linakuwa waoaji waolewaji hawapo?

Hivi kama kila mtu ana majibu ya dizaini hii nini hatima yake??

Kulikoni?

Dada umepiga ikulu mpenzi.
Mimi nadhani ni suala zima la wazazi na kumomonyoka kwa maadili.

Kama wazazi: Maadili yetu yameporomoka wengi wetu hatuna tena staha, uvumilivu, usiri wala yale maadili ya malezi mema kwa vijana wetu. Kama wazazi tunapokorofishana ndani badala ya kuyamaliza 'ndani' chumbani basi tunabwatuzana sebuleni na pengine kushikana hadharani wanetu wakisikia na kuona. Dharau, unyanyasaji tunayafanya wazi wazi. Watoto wanaona maumivu ayapatayo mzazi mmojawapo, wanashare mchungu hayo kiasi cha kujenga picha kuwa ndoa si taasis yenye furaha, upendo wala amani. Maisha yetu yanawafunza wenetu ukorofi, unyanyasaji, kiburi, dharau na jeuri. wengi wetu sio wazazi bora ni bora wazazi.

Kuna sehemu kwenye thread ya Muda hautoshi, imezungumziwa aina ya malezi tuwapayo watoto wetu kwa kisingizio cha kukosa muda kuwa busy........mamuvies wanayoangalia pasipo na uangalizi wa wazazi (age restrictions); mablogs na makolokocho mbalimbali ya kisasa yaendayo kwka jina la technolojia yanawakomaza mapema. Wazazi wengine wanafanya yasopaswa kufanyika mbele ya hadhara, tena basi hata na watu ambao si wenzi wetu, mtoto anaona anajifunza kuwa ni sawa tu kuwa na 'mashiko zaidi ya moja' tunawafunza kuthamini pesa na material things na kuwaonyesha njia ya kuvipata n.k.
 
Ni kwasababu wanaume mapepe na waliotulia wote wanatafuta wadada waliotulia wakati ni wachache, na wadada wengi nao wanatafuta wanaume ambao tayari wapo safi kimaisha hawataki kutafuta kwa pamoja.
 
ndoa zipo inategemea na choice za watu tu ,bcz saiv nasikia kuna watu wanatembea na tape,, wanavigenzo sasa utapata mtu ,ok maybe mzur au handsome but hayo hayatoshi ,hulka ,maadili ,tabia ,, bila ya hyo hakuna ndoa ,nahis hivyo kwa mm ambaye bado naish ordinary life,
 
Salama iko wana JF?

Nina jambo kidogo linanitatiza katika karne hii ya utandawazi..

Kuna hii issue ya mahusiano yaliyopo sasa....
Ukijaribu kuuliza mabinti issue ya kuoa na kuolewa utasikia majibu yao waoaji hawapo siku hizi
Ukiuliza wanaume nao jibu utasikia ni lile lile siku hizi waolewaji hawapo
Inakuwaje wakati idadi ya single wakike na single wa kiume ni wengi sana
Kwanini jibu linakuwa waoaji waolewaji hawapo?

Hivi kama kila mtu ana majibu ya dizaini hii nini hatima yake??

Kulikoni?

Bado wapo wapo kwanza mama
 
Nina jibu kwa singles wa kiume...nadhani ni wengi kwa sababu wadada singles na warembo ni wengi...ambao wanakicoki kimtindo hadi wakaka anashindwa achague yupi na kwa vigezo vipi.... Sababu nyingine ipo kwenye wimbo" bado nipo nipo kwanza". Warembo ndo kwaaanza wanazaliwa sasa commitment yanini na mateso ya ndoa wakati ukihitaji kitu unapata and for cheap.
 
Wake wazuri wapo na Waume wazuri wapo vile vile, ila ndoa inaandikwa mbinguni siku ikifika yule alosema wake hakuna na alosema waume hakuna
sikuiyo ikifika hata akiambiwa huyo mwanamme au huyo mwanamke hakufai anakua hataki kujua, na kwa mwendo wa maisha haya tunayo ishi kila mtu anamuona mwenzie kimeo, kuna wanaume wengine wanasema duh mwanamke ana simu 3 kama si kimeo nini? je mwanamme mwenye cm 1
na ina password nae tumuite nani? tuome mungu atupe mwenye kheir na sie lakini kizuri hakuna anaekijua sababu hata kizuri pia hubadilika.
 
Tatizo ni utandawazi 35%udhaifu wa kibinadam 25% kutokujiamini 40% haya ndo mamtatizo makubwa yanayomkabili mwanadam na kupelekea kufika tulipo!
 
inategemea na uliowqauliza wengi.
kama uliwauliza wa miaka kwanzia 24-26 hawa wengi bado hawajarealize haja ya kua namke.
ila kwa wengi wenye 27 and above wankua washamake sense ya kua na mke.
Pia inategemea namtu,kuna watu washakutwa sana na mikasa ya kimapenzi au kuisikia,
au kushuhudia live kwa watu wao wa karibu jamaa na marafiki. inapofikia hatua ya kuoa au kuolewa
inakua kazi sana kufikia maamuzi.

Ila kiukkweli suala la tabia nalo linachagia no kwa siku hizi.
Jamani watu wamebadilika mnoo,uthubut wa ajab wa kufanya mambo yasiyofaa
hasa kwa muolewa/muoaji. Tunatishana kiukweli.

tasia1 hapa naongelea vijana walio katika umri wa kuoa na kuolewa ..
na wala sijawauliza ila naona imekuwa ni kawaida kwa group hili kutoa majibu kama haya .
Kama hujagundua fanya uchunguzi na utaniletea majibu
 
Si kweli, mimi toka nihamie DSM miaka tisa iliyopita karibu kila jmosi nahudhuria kula mpunga wa harusi, wakati mwingine nakuwa na kadi zaidi ya moja kwa tarehe hiyo. Sasa kama hizo ndoa zinadumu au la hapo sie wahudhuriaji haituhusu.

Chapa Nalo Jr
Ni kweli uloongea mie mwenye mara kibao nashuhudia harusi za Jmos na pia mara nyingi nakuwa kwenye kamati za harusi
Lakini fanya uchunguzi wa haya ninayo kwambia
 
Sasa hili ni tusi....sema wamepungua au wako wachache!!
wa
owaji/waolewaji wapo sana tu, tatizo tamaa uchaguzi wenu tu, walio wengi wanawapenda wale wa kimjini mjini zaidi, sis du/brazamen, sasa hiyo combination hapo mikwaruzo kibao, hatima yake ni kutendana tu, ukitulia na kumtanguliza Mungu kwa hili utapata waki wa ubavu kutoka kwake...AMEN!
 
tasia1 hapa naongelea vijana walio katika umri wa kuoa na kuolewa ..
na wala sijawauliza ila naona imekuwa ni kawaida kwa group hili kutoa majibu kama haya .
Kama hujagundua fanya uchunguzi na utaniletea majibu

umri wa kuoa/kuolewa ni upi huo my dia.
 
Dada umepiga ikulu mpenzi.
Mimi nadhani ni suala zima la wazazi na kumomonyoka kwa maadili.

Kama wazazi: Maadili yetu yameporomoka wengi wetu hatuna tena staha, uvumilivu, usiri wala yale maadili ya malezi mema kwa vijana wetu. Kama wazazi tunapokorofishana ndani badala ya kuyamaliza 'ndani' chumbani basi tunabwatuzana sebuleni na pengine kushikana hadharani wanetu wakisikia na kuona. Dharau, unyanyasaji tunayafanya wazi wazi. Watoto wanaona maumivu ayapatayo mzazi mmojawapo, wanashare mchungu hayo kiasi cha kujenga picha kuwa ndoa si taasis yenye furaha, upendo wala amani. Maisha yetu yanawafunza wenetu ukorofi, unyanyasaji, kiburi, dharau na jeuri. wengi wetu sio wazazi bora ni bora wazazi.

Kuna sehemu kwenye thread ya Muda hautoshi, imezungumziwa aina ya malezi tuwapayo watoto wetu kwa kisingizio cha kukosa muda kuwa busy........mamuvies wanayoangalia pasipo na uangalizi wa wazazi (age restrictions); mablogs na makolokocho mbalimbali ya kisasa yaendayo kwka jina la technolojia yanawakomaza mapema. Wazazi wengine wanafanya yasopaswa kufanyika mbele ya hadhara, tena basi hata na watu ambao si wenzi wetu, mtoto anaona anajifunza kuwa ni sawa tu kuwa na 'mashiko zaidi ya moja' tunawafunza kuthamini pesa na material things na kuwaonyesha njia ya kuvipata n.k.

Mwanajamiione umesema vema sana na umeongea kama mzazi mwenye uchungu na hali hii ya kuporomoka kwa maadili kuanzia utoto mpaka ujana.
Nilikuwa sijawaza swala la wazazi pale wanapogombana mbele ya watoto kweli hili ni tatizo.Na jinsi mtoto anapokuwa na kuona hali ya manyanyaso kwa mama ,au mama anapata kipigo mbele ya watoto.au baba anaporomoshewa maneno machafu na mama mbele ya watoto inakatisha tamaa
Hasa pale mtoto anapokuwa na kuanza kutafakari hali ya mama kuwa anapigwa na baba au baba kutukanwa na mama .
Ni wazi mtoto ataona kama ndoa ni jehanam ,ndoa haifai .na hakuna haja ya kitu kama hicho..
Hili swala kwa sasa limekuwa tatizo katika jamii zetu..
Sijui nini hatima ya yote haya
 
umri wa kuoa/kuolewa ni upi huo my dia.

any umri kuanzia 18 +++++ Nyamayao ..
Ila mie hapa naangalia zaidi vijana walio katika umri wa 25-32 ambao bado wapo wapo tu na ukisikia maongezi yao wanasema waoaji na waolewaji hawapo
 
wa
owaji/waolewaji wapo sana tu, tatizo tamaa uchaguzi wenu tu, walio wengi wanawapenda wale wa kimjini mjini zaidi, sis du/brazamen, sasa hiyo combination hapo mikwaruzo kibao, hatima yake ni kutendana tu, ukitulia na kumtanguliza Mungu kwa hili utapata waki wa ubavu kutoka kwake...AMEN!

Asante Nyama yao be blessed
 
any umri kuanzia 18 +++++ Nyamayao ..
Ila mie hapa naangalia zaidi vijana walio katika umri wa 25-32 ambao bado wapo wapo tu na ukisikia maongezi yao wanasema waoaji na waolewaji hawapo

hiyo ni sababu nyingine inayowafanya watu wanaingia kwenye ndoa ili mradi ndoa esp wanawake, kwa kuhofia"umri" hakuna umri sahihi wa kuoa/lkuolewa, jamii yetu inatakiwa ibadilike sana juu ya hili coz ni mojawapo ya sababu zinazopelekea ndoa kuwa ndoano, mtu aliolewa coz ya kuhofia umri.
 
Sina hakika na lengo la ndoa mpenzi Nyamayao...
Ila kama lengo ni hili tulilozoea la kuanzisha familia yenye watoto, basi kuna sahihi...unaruhusu kuanzisha familia....
Hopeful hujambo....
 
Sina hakika na lengo la ndoa mpenzi Nyamayao...
Ila kama lengo ni hili tulilozoea la kuanzisha familia yenye watoto, basi kuna sahihi...unaruhusu kuanzisha familia....
Hopeful hujambo....

cjambo kabisa hofu kwako kipenzi, hivi lengo la ndoa ni kuanzisha familia? au cjakuelewa luv, hebu nidadavulie.
 
Back
Top Bottom