Ongezeko la bei lilisitishwa ili kuupisha uchaguzi mkuu tu. Hata hivyo, tupende tusipende lazima umeme upande bei tu, tena hadi JK anaondoka rasmi tusjeshangaa ongezeko la jumla kufikia 50%!
Ukweli ni kuwa hakuna njia mbadala zaidi ya kupandihsa umeme ili TANESCO iendelee kuwepo, angalia yafuatayo:-
1. Tanzania ndiyo inayoongoza kwa mfumuko wa bei katika Afrika Mashariki!
2. Anguko la shilingi dhidi ya USD tangu JK aingie mamlakani!
Tanesco hawatengenezi malighafi yoyote ya kuzalisha umeme, vifaa vyote (hata miti ya nguzo) wanaagiza nje ya nchi kwa kulipa USD, na hiyo shilingi yetu yazidi kuwa taabani kila uchao, unategemea TAnesco wafanye nini?