Jamani tumsaidie Athman Idd Chuji

Jamani tumsaidie Athman Idd Chuji

Bila kuficha wala nini kwa mtaji huu nurdin bakar, athuman idd "chuji" wa yanga na ramadhan chombo "redondo"wa azam fc
nimateja wa kupindukia huu ung.... Utawamaliza haraka saaana bora wafukuzwe yanga haraka kabla ya kuwatumbukiza wengine katika huu ulevi naamini hawa walianzia simba mchezo huu
 
Hivi sasa Chuji akijikuna anatoka vipele huku analalamika eti ni sababu ya mazoezi ya kocha mzungu
Mkuu Pengo, hapo kwenye nyekundu muhabarishaji hajakufafanulia zaidi ni kwanini...kama tatizo ni mazoezi vipi na akina Nsajigwa inawatokea kama hivyo...nauliza tu isijekuwa Chuji kachanganyikiwa na mambo ya siku hizi!...kweli tumsaidieni jamani.
 
Kama babake kashindwa, ni vigumu mtu mwingine kuweza. wenye nafasi nzuri kumsaidia ni viongozi wake klabuni.
Hatua ya kwanza ni kueleweshwa na kukubali tatizo!
 
asiyefunzwa na mamaye, hufunzwa na ulimwengu!!!
 
Kama babake kashindwa, ni vigumu mtu mwingine kuweza. wenye nafasi nzuri kumsaidia ni viongozi wake klabuni.
Hatua ya kwanza ni kueleweshwa na kukubali tatizo!

Au kama Yanga wameshindwa arudi Simba tumsaidie kama tulivyofanya kwa kocha James Siang'a.
 
Yanga Daima mbele Daima Haturudi Nyuma! Yanga oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

masanilo apo atukuelewi apo akuna swala la uyanga wala usimba apo kuna swala la chuji na mibange yake anayokula tuangalie jinsi ya kumsaidia
 
ndugu watanzania wenye nia nzuri na maendeleo ya nchi yetu hususani wapenda soka nawaomba kwa hisani yenu kuweza kumpa mawazo yaliyo mema ili kumrudisha kundini kijana athmani idd chuji mchezaji wa klabu ya yanga na timu ya taifa.

kwa mujibu wa rafikie wa karibu aitwae alela wa dodoma,ni kwamba chuji sasa amekuwa mlevi wa kupindukia kiasi cha kumfanya ashindwe kuhimili mikikimikiki ya mchezo huo uwanjani.

kwa mujibu wa bwana alela ambaye ni rafiki wa siku nyingi wa chuji,licha ya kusoma shule moja jamhuri pia walichezea timu moja ya mjimpya sc na polisi zote za dodoma,tatizo hilo tayari limefika kwa babake chuji mzee idd athman na mzee kafanya kikao cha pamoja kati ya mwanae(chuji) pamoja na ambari mtoro(mchezaji wa zamani wa cda) lakini chuji akakivunja kikao kwa kumwambia babake kuwa yeye hatumii hayo mavitu kwani walishawahi kumwona?kuona hivyo mzee idd akasema basi mungu ndiye atakaye kuongoza kama kweli hutaki kuacha hayo maulevi.

pamoja na chuji kupata pesa kiasi fulani pale jangwani hadi leo hana hata kiwanja cha kupakaziwa si dsm wala dodoma,na akifika dodoma yeye analala kwenye nyumba ya bababe pale nkuhungu.

kwa mujibu wa alela,kocha wa yanga(papic) alimpigia simu baba chuji na kumweleza hali ya mwanae na kuwa hata kuachwa kwaake timu ya taifa ni kutokana na maulevi hayo,akamwomba wamsaidie kuokoa hali ya chuji kwani anapoelekea si kwema.

hivi sasa chuji akijikuna anatoka vipele huku analalamika eti ni sababu ya mazoezi ya kocha mzungu,amesema alela.

ndugu zangu wana jamii tafadharini nawaomba sana tumuokoe huyu kijana kwani wenzie wengi kama christopher alex massawe tayari wamehathirika na hawawezi kurudia hali yao ya kawaida.


ndugu kwanza nakupa hongera kwa kuwa na moyo wa kumsaidia huyu bwana
binafsi kama binafsi labda nikueleze huku utabeba majungu na matusi jf si sehemu ya kuomba msaada kwa mwenye shida haata kidogo unaweza kuangalia huko juu wameandikaje na kuchukua ninachosema ..sasa basi isifike wakakutukania na mama yetu we jitahdi kumtafuta kwa muda wako msaidie utakavyoweza ukiendelea na kuandika utamkaribisha shetan chumbani..jumapili njema
 
Seriously speaking wachezaji wa bongo wengi hawachukulii mpira kama kazi ie walevi,indisciplined,uzinzi.
It could be wanalipwa chenji au wakishakuwa maarufu basi ndo anataka afanye kila kitu alichokikosa maishani
 
Back
Top Bottom