The Finest
JF-Expert Member
- Jul 14, 2010
- 21,605
- 6,092
Preta banaa unajua upole mwingine unaweza ukasababisha mshtuko wa moyo lol anyway ngoja nisubirie mechi ya marudiano sijui itaisha 4-0 au 0-0 au 2-1 au 1-1kwanza asante kwa kuushona moyo wangu....mpaka leo haujafumuka hata nyuzi moja.......
mambo mengine kuwa mpole bana
Una uhakika gani au ndio unafanya assumptions tu
Akili za wanaume zikoje?Akili za wanaume nazijua..
Akili za wanaume zikoje?
Inawezekana unalosema lina ukweli kwa upande fulani na upande wengine wanawake wanakuwa hawako makini.Huwa zina ubaguzi wa kijinsia.. sijui huwa ni kujipendekeza kwa wanawake??!!
Siyo uroho wa wanawake, bali aliomba msaada, kama binadamu akaamua kumsaidia. Tatizo ktk msafara wa mamba na kenge wamo. Just pray kwani pale ambapo hutaraji ndo yanatokea haya.
Mie hata mtu naemfahamu akisema nimshushe manzese nitamshusha tiptop tena mahali ambapo hakuna mtuImemkuta jamaa yangu juzi. Alimuona dada mmoja jana maeneo ya fire anasubiri usafiri wakati anamuacha mshokaji wa ofisini pale. Yule dada alimfata na kumuomba msaada kwa madai kuwa anashuka Manzese.
Kutokana na shida ya usafiri iliyokuwepo juzi na foleni jamaa kaingiwa na moyo wa huruma, akakubali. Walipofika Manzese yule dada akamwambia simama nashuka. Jamaa aliposimama dada kaanza kupiga kelele, 'nilipe hela yangu, nasema nilipe hela yangu sasa hivi! Haiwezekani unilale muda wote ule halafu usinipe hela yangu, nipe sasa hivi'.
Jamaa alishikwa nabutwaa akawa haamini anachosikia na kukiona. Na kama kawaida ya Dar, watu wakaanza kujaa kuangalia kulikoni na kulizingira gari. Mshikaji ikabdi atoe sh. 10,000 na 'kumlipa', na kuondoka kwa fedheha sana.
Jamani tuwe makini sana barabarani. Unaweza ona unatoa msaada kumbe unajiumiza.
kinacho waponzeni wanaume ni uroho na pupa zenu za kutaka kila mwanamke mrembo
haya mambo yapo na hutokea mara nyingi....cha muhimu ukiwa peke yako usimpe mtu lift na pia wakati mwingine usiku kama kuna foleni huwa wanaingia kwenye gari kwa nguvu na kudai umpe hela kama huyo dada alivyofanya......kuepuka hayo lock gari na usizoee kutoa lift hovyo
Yani naye anasubiri mpaka watu wanamjalia kibao, ajaondoa gari tu...!?
Ningekuwa mimi, break ya kwanza Mbezi kama sio kwenda kumshusha Mlandizi.[/uSIZE]
Hiyo inatokea hasa kwa wale wanawake wenye njaa wanajiuza. Ilitokea kwangu siku moja pale magomeni. Sikufunga milango wakaja jamaa wawili wananichekea nikafungua kioo kuniona wakasema ooh kumbe tulidhani ni fulani, ila si mbaya tunaomba lift mpala hapo Kigogo. Akili yangu haikufanya kazi fasta nikawambia ingieni. Pochi niliweka kiti cha nyuma nikasau kuiondoa. Bwana we walivyofika tu kwenye gari nikaona wanahangaika sana. Kucheki kwenye site mila naona mtu anafungua pochi yangu.
Dah! sijakaa sawa nikalock milango yote fasta, natafuta wapi niingie tuwachape ki-uzuri. baadae mmoja akasema ngoja tushuke hapa tusikusumbue, nikamwambia subiri hapa siyo sehemu nzuri ya kupaki, nilivyofika pale msikiti wa magomeni baada ya taa, nikaingia ndani mule, nikawaitia mwizi, eebwana walichapwa na wanachi wenye hasira, wakavuliwa nguo na hela zote walizokuwa nazo na wallet yangu wakarudisha. Niliwaacha mule wakipiga kwata la ijumaa.
ki ukweli kama mtu humjui, usijifanye msamalia mwema utakutoka puani.