Hiyo inatokea hasa kwa wale wanawake wenye njaa wanajiuza. Ilitokea kwangu siku moja pale magomeni. Sikufunga milango wakaja jamaa wawili wananichekea nikafungua kioo kuniona wakasema ooh kumbe tulidhani ni fulani, ila si mbaya tunaomba lift mpala hapo Kigogo. Akili yangu haikufanya kazi fasta nikawambia ingieni. Pochi niliweka kiti cha nyuma nikasau kuiondoa. Bwana we walivyofika tu kwenye gari nikaona wanahangaika sana. Kucheki kwenye site mila naona mtu anafungua pochi yangu.
Dah! sijakaa sawa nikalock milango yote fasta, natafuta wapi niingie tuwachape ki-uzuri. baadae mmoja akasema ngoja tushuke hapa tusikusumbue, nikamwambia subiri hapa siyo sehemu nzuri ya kupaki, nilivyofika pale msikiti wa magomeni baada ya taa, nikaingia ndani mule, nikawaitia mwizi, eebwana walichapwa na wanachi wenye hasira, wakavuliwa nguo na hela zote walizokuwa nazo na wallet yangu wakarudisha. Niliwaacha mule wakipiga kwata la ijumaa.
ki ukweli kama mtu humjui, usijifanye msamalia mwema utakutoka puani.