Jamani tuwe makini tunapotoa 'lift' za magari.

Jamani tuwe makini tunapotoa 'lift' za magari.

Hivi na kuomba lift pia hua hamuogopi??Mi kama mtu sio ndugu au rafiki yangu siombi..sitoi wala sipokei lift yake.Kubalini kuonekana wachoyo mbaki salama...na wadada wazuri wanajua udhaifu wenu kwahiyo wafungieni macho kabla hamjaamka mtaroni bila hata pensi!
 
Nilimpa lifti mzee mtu mzima nikambamba ananipekua wallet yaani alifedheheka sana na bado tunaishi mtaa mmoja
 
Ilikuwa ghafla na hakutaraji. Alishikwa na butwaa kiasi kwamba watu walipoanza kuzingira gari alipata hofu kutokana na mfadhaiko. Mdada anaongea kwa kujiamini utafikiri katoka naye nyumba ya wageni kikweli. Pale Manzese angekomaa naye angepoteza zaidi ya hiyo Tshs 10,000/=.
Huyo jamaa yako naye yupo too slow...! Yani anashikwana butwaa plus mfadhaiko!? Mjini hapa....! Ooh! Au kakulia Peramiho!?
 
Pole yake, kwa kweli inatakiwa umakini sana katika ishu hiyo ya kutoa lifti, sio kila mtu ni mzuri!
 
Huyo jamaa yako naye yupo too slow...! Yani anashikwana butwaa plus mfadhaiko!? Mjini hapa....! Ooh! Au kakulia Peramiho!?[/

Kasoma hizi hizi za kwetu. Kama ulishawahi sikia afadhali unaweza soma alama. Bt 4 first day, ningumu. Unakuwa unabishana akili yako,
 
Back
Top Bottom