Elections 2010 Jamani vipi kuhusu HALI YA AFYA YA MREMA?

Elections 2010 Jamani vipi kuhusu HALI YA AFYA YA MREMA?

Huyu mheshimiwa anaugua pia ugonjwa wa kisukari.. Anyway, ni ugonjwa sugu na mgumu sana kukabiliana nao, especially kwa mazingira kama ya kwetu hapa Tz.
Nataraji ata-improve baada ya kuukwaa tena uheshimiwa, maana ndiyo alikuwa unapigania kwa udi na uvumba, hadi akasahau kumpigia debe mgombea wa urais wa tlp.
FYI, watu wa Vunjo wamempa ubunge ali ajipatie kaulaji walau na ka-pension--otherwise hawategemei kupata chochote cha maendeleo!!
 
Huyu yuko fiti tu!
Mumewahi kumsikia kaanguka jukwaani hata siku moja?
 
Mzee Mwinyi afya yake ya wastani kwa umri wake (84 years?). Na yeye anafanya mazoezi ya nguvu na ana nidhamu kweli.

Kuna kipindi nilikuwa Zenj na yeye alikuwepo huko kila asubuhi alikuwa anapita na bodigadi wake pale mbele ya nyumba niliyokuwa naishi amepiga tracksuit yake anatembea kimazoezi.

Kwa hiyo nimempa heshima yake.
 
Kweli Murema wa Lyatonga mzee wa vibomu afya yake inaporomoka... Nadhani CiCieMu walimfanya vibaya huyu mzee. I suspect something. Kuna wakati kipindi kilee waliwahi kukamata gari yake kwa muda wa wiki nzima. Gari ikashinda usalama wa Taifa, then wakamrudishia...walichoweka humo ndani ya gari ndicho kinachomtesa Murema. Yaweza kuwa Kisukari kweli...lakini CiCieMu waweza fanya lolote.
 
Huyu mzee ana kisukari muda mrefu!! Huenda hili likawa moja ya sababu, pia na uzee; bila kusahau choka mbaya ya fweza!!!

Ukiona mtu mzima analialia ujue mamba yamefika shingoni, aliomba CCM wasiweke mtu Vunja, wamuachie...:smile-big:
3.jpg
 
Kama mnakumbuka siku ile alivyokuwa anacheza mayenu pale Dododma kwenye mkutano wa CCM na jinsi alivyokuwa anamwagia sifa Mkwere, basi ujuwe njaa haina heshima, Lyatonga siyo mgonjwa kiivyo hiyo ni njaa tu,ngojeni baada ya miezi miwili kama atakuwa hivyo. Adui yako muombee njaa.
 
Mh!afya ya mtu ni siri yake!ingawa hali inaonyesha si nzuri!!
 
ameenda bungeni ili apate fedha za kutibiwa nje na kukuza pension yake kwa familia
 
Sina nia ya kuchimba mtu kwa saana, lakini picha za hivi karibuni za huyi Muhishimiwa Mrema naona kama mzee kazoofu hivi ama macho yangu tu?

Alishasema kua anayetaka kujua kama afya yake ina mgogoro amuulize mke wake:smile-big:!
 
huyo akiingia saluni ya maana akapigwa sopsop halafu akawa anahudhuria mnadani kwa ajili ya dozi ya michemsho daily, hasa ule wakati wa bunge la bajeti, wiki 3 tu mtaona anatoka shavu dodo
kuna jamaa alimpeleka Mrema oceanic akamnunulia bata Mrema alifurahi sana ikabidi jamaa amuagizie na take away. sasa najua atakuwa anaenda pale mara kwa mara kwa ajili ya bata.
'aiseee mtu wa jikoni, fanya fanya bata aisthee'
 
Mzee Mwinyi afya yake ya wastani kwa umri wake (84 years?). Na yeye anafanya mazoezi ya nguvu na ana nidhamu kweli.

Kuna kipindi nilikuwa Zenj na yeye alikuwepo huko kila asubuhi alikuwa anapita na bodigadi wake pale mbele ya nyumba niliyokuwa naishi amepiga tracksuit yake anatembea kimazoezi.

Kwa hiyo nimempa heshima yake.

Na hakupitia jeshini, je angepitia akawa na cheo cha Luteni Kanali!
 
The most effective comeback to an insult is Silence:A S-cry:
MH!me simo

 
wananchi waliomchagua wanadai kwa aliyowafanyia kipindi cha nyuma yeye ndiyo mbunge wao mpaka afe kwa uzee au ugonjwa hivyo usipate shida analipwa fadhila na watu wake.
 
Kuchoka kachoka, tena kama angelambishwa sakafu kama Masha... naamini KCMC wangepokea mgeni. ila Naamini wamesha pewa Advance ya sitting mjengoni kwa maana hiyo huenda visupu na mtori pale mnadani havimpigi chenga, hivyo tuwe na subra huenda yale mashavu ambayo yalishaanza kugongana na meno yatajitokeza. sema kwa sasa hapo njengoni nafikiri anaongoza kwa kuchoka.:coffee:
 
Back
Top Bottom