Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Akina baba hufanya hivo kwa ajili ya nani?Kuna mtoto wa jirani yangu alimwita kijana anaye waletea maziwa asubuhi baba
baba anaondoka nyumbani mtoto amelala anarudi mtoto amelala
Upendo kwa mama lazima
angalia mtetea na vifaranga vyake mvua ikinyesha ndani ya mbawa zake jogoo yuko wapi?
Mama anakunyonyesha, anakutunza, anakujali kuliko baba, Lakini si kwamba Baba hapendi kuwa karibu kama Mama hapana anakuwa hana muda wala nafasi hiyo hawezi kukunyonyesha, hawezi kukuogesha, hawezi kukulisha chakula mara kwa mara, inaweza kutokea mara moja moja sana.
Hii inatokana na kwamba mara nyingi mama ndie anayekuwa karib zaid na wanae kuliko baba nando maana hata mtoto anakuwa na ujasiri zaid wa kuexpress shida zake kwa mama kuliko baba.(kwa wapenz wa bios nafkiri mtakumbuka ya kwamba ma mjamzito anapojifungua huwa ana release homoni ambayo ina mwifluensi kuwa karib na mwanae)
Ukiangalia kwa undani utakuta wote wale waliokuwa wantoa shukurani zao kuzielekeza kwa mama,historia ya maisha yao wamelelewa na mama tu,either baba amefariki au walitengana muda mrefu inaweza ikawa hata tangu ya utoto,kwa hiyo mapenzi waliyokuwa ni ya upande mmoja zaidi
Hebu wana jf tuliongelee hili, kwa ushuhuda nilionao naona watoto wana mapenzi sana na mama zao kuliko baba. Hebu tuangalie mifano michache, nyimbo nyingi zinazoimbwa dedication ni kwa mama, watu wakipewa nafasi ya kutoa shukrani mara nyingi mama anatajwa tena bila kumuhusisha baba, juzi tuzo za kili wasanii wengi walidedicate tuzo kwa mama, tukiulizana hapa kati ya baba na mama nani unampenda wengi tutajibu ni mama. Mimi najiuliza kwa nini baba mara nyingi hana nafasi mioyoni mwetu? Jamani tatizo liko wapi?
mmh! Mbona me naic baba hapewi nafac kubwa sababu muda mwingi ana dedicate kwa small house or smtym anaitelekeza completely nyumba yake. Ndo mana hatuwapendi
Wewe tu kwa baba yako, nampenda mama na nampenda baba. Bila baba nisingepata nafasi niliyonayo mpaka sasa na mapenzi niliyo nayo kwa mke wangu na watoto. Kwa kadili baba na mama walivyoishi ilinipa chachu ya kujuwa wajibu wangu kama baba na kujitambuwa kuwa ni wajibu wangu kuijenga na kulinda familia, kuwa muhimili mkuu na mfano wa kuigwa hata kwa watoto wangu wa kiume wanavyopaswa kuishi na wake zao huko baadaye.
hii thread imerudiwa???
"Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako." ss anayemuheshimu mama peke yake amri ya 5 inajieleza!!!