Jamani wanajamvi wawezanipa maoni yako hapa!!!!

Twaa

Member
Joined
Mar 3, 2011
Posts
46
Reaction score
10
Napenda kuwaomba wanajamvi mnipe angalau cha kufanya ili nipate sponsorship ya kwenda kusoma diploma in electronics and Telecommunication engineering! Jamani naombeni msaada wenu jamani! Mimi nimeshahitimu elimu ya kidato cha sita na alama 11 yaani division two ya point 11 kwa mchepuo wa sayansi yaani PCM(PHYSICS , CHEMISTRY NA MATHEMATICS) Ila mimi natokea katika familia maskini mno yani haina hata refa wa kuniwezesha na nipo tayari kuwania mwanafamilia wa atakaeniwezesha kupata sponsorship au atakaenisponsor! nimejaribu kusaka pesa lakini kwa kweli nimeshindwa kabisa! Naombeni msaada wenu jamani WANAJAMVI!
Hata kama ni vigumu kwako kutoa ushauri nawaomba jamani mniambie hao wanaopata sponsorship kutoka SBL wanafanyaje ndio wapate? Mimi mwenzenu mwanajamvi naombeni msaada wenu plz!!!! Kwa upendo zaidi nakuomba uniPM!!!!
 
Mbona una matokeo mazur tu mkuu,omba kusoma degree na uombe mkopo loans board.
 
Kwanini umependa kwenda kusoma diploma? Nakushauri,nenda posta,library ya mkoa au ofisi afisa elimu wilayani na uombe "Admission Guidebook" na utajionea mwenyewe vyuo kibao vyenye programmes unazozitaka na kipaumbele cha serikali kwenye loan. Programe kama yako 100% loan.Fanya hvyo kwanza kaka.Mi mwenyewe nipo kwenye situation kama yako.Mwaka jana niliomba nikakosa loan,mwaka huu nataka niombe education tu.
 
Mimi nimependelea diploma kwa sababu ukishapata degree ya engineer utakua hauna competition kwenye ajira kwani utakua fiti theoretically lakini practically unakua shalo! Na pia diploma unakua umesoma kipractical zaidi na utakua na competent kwenye ajira yako au yeyote ile nje au ndani ya nchi !
 
We umemaliza form six mwaka gani? kwa maana tunasubiri matokeo ya form six.
 
mie nlimaliza form six mwaka 2010! lakini umeielewa thread yangu?
 
Mimi nimependelea diploma kwa sababu ukishapata degree ya engineer utakua hauna competition kwenye ajira kwani utakua fiti theoretically lakini practically unakua shalo! Na pia diploma unakua umesoma kipractical zaidi na utakua na competent kwenye ajira yako au yeyote ile nje au ndani ya nchi !

Nani amekudanganya!!!!
 
Please give us your contacts that we can educate you, acha kuhangaika.
 
mie sijadisco mkubwa! Yani kama ningekua nimeenda nikadisco inaama ningekuja hapa jamvini na kuomba ushauri? Mimi sio mtu wa hivyo! Mgonjwa anataka kinga na tiba kama ipo!
 
Kaka hyo yako ngumu! Sifahamu kama kuna vyuo vya diploma vinavyopata sponsorship kutoka serikalini.Kwa watoto wa wakulima kama sisi tunahangaika kutafuta programmes zinatoa loan 100% na alternative yetu ni diplma ya education. Ungekuwa unatoka familia maskini usingechagua pakusoma,badala yake ungefuata mtelemko.
 
Ungeomba SUA BSc Agric Engineering ungepata sponsor 100%.
Mpendwa, beggars cannot be choosers. Katika stage hii nakushauri upate elimu yoyote manake uko financially desperate. Wale unaowaona bank wanahesabu hela za wenzao wamesoma hadi nutrition, engineering, sijui hr! Kila la kheri
 
Nashukuru sana mpendwa! nshakuelewa beggars cannot be choosers! I will take action on it!
 
Kaka hyo yako ngumu! Sifahamu kama kuna vyuo vya diploma vinavyopata sponsorship kutoka serikalini.Kwa watoto wa wakulima kama sisi tunahangaika kutafuta programmes zinatoa loan 100% na alternative yetu ni diplma ya education. Ungekuwa unatoka familia maskini usingechagua pakusoma,badala yake ungefuata mtelemko.

Vyuo vya diploma vipo, ila issue ni ada! Je wajua D.I.T? NAPENDA SANA ELECTRONICS ILA HALI YANGU YA KIFEDHA ILIVYO yanipasa sana nibadike!
 
Back
Top Bottom