UKI
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 691
- 173
Nilikuwa naangalia BGT (british Got Talent) mashindano haya ni mahususi kwa waingereza kutafuta kipaji chochote ulichonacho iwe kuimba,dancing, kucheza na mbwa na kila kitu unachokijua,(mwaka jana mbwa ndio alishinda jinsi anavyochezeshwa mziki na kufualitia kwa vitendo) Leo nimeshangaa nimeona wamama wawili wamejitokeza wanajiita Tanzshake wanaishi uingereza wanatokea Tanzania wanasema wanavipaji vya kukata mauno! wameserebuka ile mbaya,mwenye show hii ni simon cowel mzee wa X factor amewakubali wamepita kwenye round ya kwanza wanaenda round ya pili mshindi atapata £500,000 kama tsh 1,275,000,000/= ila kushinda hawawezi kushinda ingawa wameshajulikana maana kwenye page yao ni full gumzo hayo mauno ya watoto wa kimatumbi,