Tetesi: Jamatini Dodoma na kituo cha Daladala

Tetesi: Jamatini Dodoma na kituo cha Daladala

Habari ya siku nyingi sana wanajamvi wenzangu,nimepita hapa Dodoma kikazi kiukweli sijaelewa mji mzuri kama huu unakosa stendi ya Dala dala,katika kuuliza nikaambiwa pale jamatini ndipo dala dala zote zilikuwa zinaishia pale lakini tatizo ni moja kuna watu wawili wanatunishiana misuri ambao ni Mkurugenzi wa Jiji na Boss mmoja wa Railway,kiukweli watu wanateseka kwa ujinga wa watu hawa(Tasisi hizi mbili)badala ya kufikilia maendeleo ya jiji la Dodoma wao wanafilia mambo yao,inakuwaje stendi ipo tayari na kila kitu kipo lakini haitumiki?naamini watu wa Dodoma watakuja hapa kutujuza vizuri.
Nadhani railway wamechukua eneo lao.....kwahiyo stendi kuu pamoja na stendi ya daladala iliwalazimu kupisha eneo hilo.
 
Mkurugenzi wa jiji ndiye tatizo. Lile ni eneo la shirika la Reli, lakini uongozi wa jiji unataka kuchukua mapato yote bila shirika la Reli kupewa chochote kama wamiliki wa eneo. Wewe ungekubali kuachia mapato toka kwenye eneo lako?!
Kwani wakiyachukua hayo mapato wanayarudi nayo majumbani kwao? Ni mambo ya ajabu mno kwa taasisi za serikali kugombea mapato (against each other), si ichukue taasisi yoyote tu
 
Kwani wakiyachukua hayo mapato wanayarudi nayo majumbani kwao? Ni mambo ya ajabu mno kwa taasisi za serikali kugombea mapato (against each other), si ichukue taasisi yoyote tu
Dah, tuna safari ndefu bado.
 
Ata kama eneo ni railway lkn ujue manispaa ya jii ilikuwa imeshawekeza pale kwa kujenga stendi ya hiace nzuri sasa kuifunga eti isifanye kazi nawakati pale ni mjini kabisa opposite na office za tanesco na benki ya posta ni karibu na nyerere square karibu kabisa na Office za Lapf sasa unaamishia stendi kule sabasaba stendi imejaa vumbi na mashimo alafu unajisifu kwamba unawatendaji unawategemea kutatuwa kelo za watu wakati wanashindwa ata kutatua jambo dogo kama ili.
 
Back
Top Bottom