Tetesi: Jamatini Dodoma na kituo cha Daladala

Nadhani railway wamechukua eneo lao.....kwahiyo stendi kuu pamoja na stendi ya daladala iliwalazimu kupisha eneo hilo.
 
mkuu siyo stendi ya daladala tu, umeshafika nanenane stendi kuu? pote ni vuluvulu tu.
Hivi nane nane ndio ile stendi yenye vumbi tupu? Kama ndio pale aisee inasikitisha sana
 
Mkurugenzi wa jiji ndiye tatizo. Lile ni eneo la shirika la Reli, lakini uongozi wa jiji unataka kuchukua mapato yote bila shirika la Reli kupewa chochote kama wamiliki wa eneo. Wewe ungekubali kuachia mapato toka kwenye eneo lako?!
Kwani wakiyachukua hayo mapato wanayarudi nayo majumbani kwao? Ni mambo ya ajabu mno kwa taasisi za serikali kugombea mapato (against each other), si ichukue taasisi yoyote tu
 
Kwani wakiyachukua hayo mapato wanayarudi nayo majumbani kwao? Ni mambo ya ajabu mno kwa taasisi za serikali kugombea mapato (against each other), si ichukue taasisi yoyote tu
Dah, tuna safari ndefu bado.
 
Ata kama eneo ni railway lkn ujue manispaa ya jii ilikuwa imeshawekeza pale kwa kujenga stendi ya hiace nzuri sasa kuifunga eti isifanye kazi nawakati pale ni mjini kabisa opposite na office za tanesco na benki ya posta ni karibu na nyerere square karibu kabisa na Office za Lapf sasa unaamishia stendi kule sabasaba stendi imejaa vumbi na mashimo alafu unajisifu kwamba unawatendaji unawategemea kutatuwa kelo za watu wakati wanashindwa ata kutatua jambo dogo kama ili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…