Jambo baya ambalo halisemwi na kukemewa wakati wa Ramadhan

Jambo baya ambalo halisemwi na kukemewa wakati wa Ramadhan

Dr Rutagwerera Sr

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2011
Posts
5,809
Reaction score
11,462
Ningependa kuandika hili juu ya wakati tulionao wa mwezi wa Ramadhan.

Nimegundua na kujionea sana wakati huu ndio wakati chakula kingi hupikwa majumbani na watu wakakichezea na kisha kukitupa. Nimealikwa, na hali kadhalika nimejionea kwa jamaa zangu pia namna chakula kingi kikipikwa na kuwashinda walaji.

Hoja yangu ni kwanini watu hupika vyakula vingi na mwisho vikawashinda na kuvitupa.?Binafsi naona moja ya faida ya kufunga wakati huu ni kula kiasi kwa lengo la kupata manufaa ya kiafya, kinyume ni kana kwamba kufunga ni adhabu. Unakuta familia ya watu wachache lakini inapikwa futari mithili ya shughuli ya watu wengi.

Tubadilike ndugu zanguni. Kuchezea chakula ni moja ya tabia mbaya sana. Na hili liende na kwa watu wengine wenye tabia kama hii.
 
Hao wanafunga au wanashinda na njaa
 
Kuna wengine wanaita matajiri wenzao kufuturu badala ya kuita wale wasiokuwa na uwezo.

Matokeo yake wakija matajiri hakuna mlaji zaidi ya kugusagusa tu futari na kuacha.

Hii si sawa kabisa..!
 
Inakuwa aje kipindi cha mfungo wa chakula, ndio kipindi cha kula vizuri au/ na kingi zaidi? Maana hata sokoni, wachuuzi wanajua wakati wa Ramadan ndio muda wa neema! Haileti mantiki.
 
Back
Top Bottom