bakundande jr
JF-Expert Member
- Oct 22, 2021
- 507
- 672
Haabari za muda wanajukwaa, bila shaka ni wazima wa afya na pasi na shaka mko katika majukumu mbalimbali ya kulijenga taifa letu.
Bila kupoteza muda moja kwa moja niende kwenye mada husika.
Katika maisha ya kusoma kuna kipindi unaweza soma au kusikia mada fulani na kuitafsiri tofauti na maana yake.
Kwa mfano: Nakumbuka nikiwa kidato cha tatu hapo bado navaa shati nyeupe ya mikono mifupi na suruali nyeusi ya kitambaa. Siku moja mwalimu wa History alikuja darasani mada ya siku ilihusu vita ya kwanza ya dunia(WW1) akazungumzia hatua zilizochukuliwa na mataifa baada ya vita hizo
Moja ya pointi alizozitaja ilikuwa ni FORMATION OF LEAGUE OF NATIONS baada ya kusikia tu hiyo point nikatabasam nikasema ewaaa leo Madam kayakanyaga. Kwa ujasiri nikanyoosha mkono na kutaka kuilezea nilipochagulia tu nikaseka hiyo LEAGUE OF NATIONS ni mashindano ya kombe la dunia (WORLD CUP) nakusema kuwa lengo kuu la kuanzishwa kwake ni kuleta watu pamoja.
Aisee mwalimu na darasa zima waliangua kicheko kisha Madam akasema mpigieni makofo huyoo baada ya hapo akaanza kuelezea. Aisee siku hiyo nilishinda nimenywea sana.
Vipi Mdau kwa upande wako ni kipi uliwahi kufikiria kipindi hicho na kikawa tufauti na maana ya jambo husika.
Naomba kuwasilisha.