Jambo gani umewahi lifanya kwenye mapenzi ukajutia

Jambo gani umewahi lifanya kwenye mapenzi ukajutia

Kwa kweli, kwa uaminifu kabisa kulingana na maoni yangu ya unyenyekevu, bila kuwa na hisia na bila kumkosea yeyote anayefikiria tofauti na maoni yangu, na bila kuficha mawazo yoyote akilini mwangu, na bila uwongo kwa ukweli halisi, kwa akili yangu wazi na moyo wangu safi, nikiweka wazi kila kitu kilichojificha ndani yangu kwa muda mrefu ambacho sikusema kwa sababu nilikuwa na wasiwasi. Lakini leo, kwa kukusanya ujasiri na motisha yote, nataka tu kusema kwamba mimi kimsingi naona na kufikiria kwamba Sina lolote la kusema.Asanteni.
 
Aisee mimi nilikuwa nafukuzia manzi (bonge la pisi ana tako sura usiseme) ila alikua na mchizi wake akawa ananikazia japo kwa mbali kulikuwa na matumaini kidogo.

Sasa manzi akashika mimba ya mchizi wake mimi sijui na hapo ni kama miezi miwili namfukuzia hata game sijapewa bado. Sasa kabla ajamwambia mwamba ana mimba yake jamaa akatoa boko akazingua wakaachana.

Mwanaume nikapewa nafasi lakini akanichana ana mimba ya ex wake na jamaa hajui ila yuko tayari tuwe wote kwa sasa kwa sababu kaachana na jamaa mazima

Hapo nikakumbuka maneno ya mzee wangu aliniambia ukiniletea mwanamke ana mtoto lakini sio wako sitokukatilia ila utakuwa umenidisappoint sana wanawake wote waliopo ufate mwenye mtoto?

Ikabidi nimwambie live manzi mimi maishani sijawahi kufikiria kuoa mke tayari ana mtoto so kama kweli yuko tayari aitoe kwanza mimba tuanze upya wote. Manzi akasema atajifikiria then ataniambia

Basi kesho yake dem akanichana yuko tayari kuitoa ili tuwe wote kidume nikazama pharmacy kutafuta dawa za kutoa mimba nikampelekea kwake nikamuachia akameza mimi nikarudi home maana hakutaka akati anameza mimi niwepo

Baada ya kama lisaa maumivu ya tumbo yakawa makali kwa kujitia najali nikamfata nikamleta ghetto ili niwe nampa kampani asiwe peke yake

Kiukweli ule usiku ulikuwa mrefu sana maana sikulala mtu analalamika tu tumbo kulivyokucha nilishukuru sana mungu lakini ile hali ikaendelea kumbe haikutoka fresh ikabdi nitafute hospitali wakamsafishe ndio akaja akapona sasa.

Kiukweli nilijiona fala nikawaza huyu angekata moto humu ndani ingekuwaje maana jela ilikuwa inaniita maana aliishi na maumivu kwangu kama wiki mpaka kusafishwa
Dhambi ya kuua kiumbe kisicho na hatia itakutafuna miaka yako yote kuanzia hapa duniani mpaka ahera.
 
Kipindi cha ujana, nilisafiria Penzi kwa binti wa mkoa fulani, mkoa ambao niliutamani sana kuutembelea kutokana na sifa zake wanazoujaza watu.

Basi kwakuwa huyo manzi anaishi huo mkoa nikaona hapa ndio fursa ya kumaliza ndege wawili kwa jiwe moja, kidume nikakata tiketi kusafiria penzi lisilo na matumaini.

Picha linaanza nmekaribia stendi napiga simu, manzi haipokei, tuma sana meseji bado manzi haitaki kujibu, wee nikaona asinitanie nikatuma sana sms za vitisho na malalamiko lkn wapi ndio kwaanza simu ikazimwa[emoji28].

Basi matumaini ya kupata penzi yakaishia hapo, nikashuka kwa basi kinyonge sana huku nikijipa matumaini labda atapokea simu , nilikaa sana stend zaid ya saa zima kila nikipiga simu haipatikani na ikipatikana haipokelewi, ase nikaona huu upuuzi kama plan A imefeli wacha niendelee na plan B haswa ambayo ilikuwa ni kufanya utalii wa huo mkoa, usiku huo huo nikachukua usafiri huyoo Hotelini nkamalizia usingizi wangu huko na asubuhi na mapema nikaanza sasa Rutii za chocho to chocho kujionea kwa macho sifa za huo mkoa watu wanazoujaza,

Basi siku ya 2 nikageuza huku machungu ya kukosa penzi yakiwa yamekauka uku nikijipa matumaini kuwa namimi nimeshautembelea huo mkoa "X" unaotajwa sana na hamu yangu ikaishia hapo, kwa hakika ulikua ni ujinga wa aina yake yaani nilikula nauli yangu mimi mwenyewe sio mbaya[emoji28].
Mkuu huo mkoa utakuwa Tanga, yani sipati picha ulivokuwa umekamia mizagamuo
 
Baada kuachna tuuu haikupita at wiki ashampt bwana mpya tena rAfk angu duuuh😏😏😒😏😒
 
Back
Top Bottom