Jambo Jema kutoka Afisa yoyote wa Polisi..

Jambo Jema kutoka Afisa yoyote wa Polisi..

kaka_mkubwa

Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
40
Reaction score
75
Habari za waungwana.
Pamoja na kuwa kuna msemo kuwa samaki mmoja akioza basi wote wameoza, inaweza ikawa tofauti.
Naomba kuuliza je, kuna wakati umekutana na afisa/askari wa polisi akakutendea kwa utu, heshima na huruma?
Kuna mifano mingi, ikiwemo kuwapa chakula mahabusu ambao huwa hawajaletwa chakula kwa muda mrefu... n.k. huwanunulia chakula kutoka hela zao za mfukoni.
Je, wewe umekutana na kisa kipi kilichokuonyesha taswira ya utu, heshima, na huruma kutoka kwa afisa/askari wa polisi?
Karibu
 
Kuna wp nilimpelekea moto mwaka jana akaninunulia boxer 3, singred 3 na soksi pea 2.
Rip wp leti, nitakukumbuka.
Ilikuwaje mkuu?
Funguka basi.
Asante sana WP Leti kwa wema wako. Pumzika kwa amani. Wema ulioutenda uzao wako/uwapendao waje wale matunda
 
Na wao Ni binadamu Sasa akuna raia wakorofi wasiopenda kutii Sheria so inabidi wawe wakali na wakatili yaani wavae sura ya kazi,ya Simba ili wawe wapole. Hata wewe home kwako inabidi uwe mkakisi ndio wanao ama wife atakuelewa
 
Mie walinipenda sana hadi wakanificha mahabusu kunisaidia usalama wangu
 
Habari za waungwana.
Pamoja na kuwa kuna msemo kuwa samaki mmoja akioza basi wote wameoza, inaweza ikawa tofauti.
Naomba kuuliza je, kuna wakati umekutana na afisa/askari wa polisi akakutendea kwa utu, heshima na huruma?
Kuna mifano mingi, ikiwemo kuwapa chakula mahabusu ambao huwa hawajaletwa chakula kwa muda mrefu... n.k. huwanunulia chakula kutoka hela zao za mfukoni.
Je, wewe umekutana na kisa kipi kilichokuonyesha taswira ya utu, heshima, na huruma kutoka kwa afisa/askari wa polisi?
Karibu
kuna day moja tulikuwa na IT,yule askari baada ya kutusimamisha na kukuta tumebeba mzigo,akaanza kutupa semina ya zuio la ubebaji mzigo,na kwamba kwanini haitakiwi kubeba mzigo.Baada ya kumaliza kutuelekeza akatuambia tuende,hakutupiga faini,ila akaturuhusu.Nikasema binadamu hawa ni wachache sana,nikampa 5,000 ya asante nikiamini ni vyema kutambua moyo wake katika haki ili aendelee kuwatendea haki wengine.

Naamini mwingine angefamya kuwa sehemu ya kushusha adhabu bila haki ya kuelekeza.

Mungu ambariki sana.
 
Back
Top Bottom