Jambo Leo lanunuliwa na Rostam, lahamishiwa New Habari

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
239
WanaJF;

Habari za uhakika nilizopata kutoka New Habari ni kwamba Rostam kalinunua gazeti la Jambo Leo kuanzia jana. Utayarishaji wa hilo gazeti unahamia Sinza katika newsroom za New Habari na litakuwa linamilikiwa na kampuni hiyo.

Nawasiliasha!
 
Nasikiavyo lilikuwa linaendeshwa kwa ruzuku kutoka serikalini, na sasa ruzuku hiyo imekatwa ghafla kutokana na serikali kuwa hoi kifedha.
 
lilikuwa haliuzi -- ni hasara tupu. Hivyo limepatiwa 'soft landing' na Rostam.

Ila kinachonishangaza ni kwamba pale New Habari nako ndiyo tu wameanza kupata nafuu kifedha baada ya kuachana na sera za kutetea ufisadi, sasa mzigo huu tena!

Wanahabri wote pale New Habari wamepigwa na butwaa!
 
Halafu niliona juzi gazeti moja limeandikwa JAMHURI likiwa linafanana fanana na Mtanzania kwa sura niulize ndo Rostam kaamua kulibadili gazeti lake ili liwe na mvuto au ni gazeti jingine?Kwa walioliona tafadhali nijuuzeni
 
Shida nini,si mngenunua nyinyi kama hamkutaka Rostam anunue?Wenzenu wanafanya biashara nyinyi mnafuatilia umbeya!
 
Mikakati ya 2015. Eti Malaria Sugu anajifanya hajui hilo??
 
WanaJF;

Habari za uhakika nilizopata kutoka New Habari ni kwamba Rostam kalinunua gazeti la Jambo Leo kuanzia jana. Utayarishaji wa hilo gazeti unahamia Sinza katika newsroom za New Habari na litakuwa linamilikiwa na kampuni hiyo.

Nawasiliasha!

Acha maneno ya kwenye kahawa, rostam hajanunua gazeti, gazeti limenunuliwa na kampuni ya new habari na si vinginevyo1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…