Jambo lililomtesa Hayati Dkt. Magufuli ni mkataba wa Dowans na Symbion ambao Mzee Kikwete alisaini wakati wake


Huyu mwamba kupotea kina Azory, Sanane, Lijenje nk. Kushambuliwa kina Lissu. Watu kuokotwa kwenye viroba. Kuuwawa kinyama kwa akina Mawazo.

Yote hayo hayakuwahi kuwa kitu kwake ila mkataba wa Dowans na Symbion?

Maajabu ya Mussa!

Watu wasiokuwa na mioyo ya kibinadamu kama huyo na wasipewe tena nafasi za uongozi.

Bure kabisa. Hakuelewa alikuwa na majukumu gani muhimu zaidi kama rais.
 
Katiba nyingine yenye maboresho mhimu ni dhahiri inahitajika Ili kupunguza baadhi ya mambo yanayoonekana kutajwa tajwa Sana. Wanaosema Haina maana , maendeleo kwanza watambue tutaendelea kusikia hayahaya miaka na miaka...hata JPM angeruhusu mchakato wa katiba mpya uishe saiv angetuacha ktk mazingira magumu...
 
Mbona munatuchanganya,tulikubaliana kua Mama kawekwa na Jk na ndio anamuenda.
Leo Jk anataka kumuangusha Mama tena 2025.
Hatujui tusimamie wapi sasa
 
hata yule mchora picha kukamatwa inaonyesha order imetoka kwa JK jicho la tatu.

JK itakuwa ana nguvu sana na part ya deep state
 
Mtajijua wenyewe, sisi kila siku tunapigia kelele KATIBA MPYA mnatuona wasumbufu. Pambaneni na hali zenu tu.
 
Tafsiri yake ni kuwa JPM alikua mnafiki akashindwa mdhibiti bwana huyu....bro hapa umepuyanga na conspiracy zako za kijinga
 
Kuna mama mmoja ana kampuni ya mawakili kampuni yake ilikuwa inawatetea Dowans na kesi hata haijaisha lkn cha ajabu serikali hii imemteua kuwa kati ya menejimenti ya tanesco cjui ni kukosea au mpango mkakati hv kweli adui yako unamueka jikoni kweli? Huko.mbeleni sijui umeme wetu utakuwaje Mungu ibariki Tanzania tuendelee kuiombea Nchi yeTu.
 
Samia alitetewa na Jeshi asingekuwa Mkuu wa Majeshi kusema wao wanazingatia katiba angetupwa mbali! Hakuwa JK, kwani hata kwenye Kamati Kuu hakuingia, na akiingia ni mwalikwa tu.

Kikwete huwezi mtenga na JPM hawa walijuana. Nyakati za uongozi wa Kikwete hasa awamu ya pili Magufuli aliwekwa karibu sana na Kikwete. Hata kama mnakumbuka alie mpa ushauri wakati anaumwa Kikwete alikuwa ni JPM. Kikwete alikuwa ana muandaa JPM. Watu wanadhani ati iliibuka tu.

Nachojua Kikwete anaonewa sana. Kikwete si kiongozi fisadi na hakulelewa hivyo. Na hakuwahi kuiibia nchi. Yule mzee wanamuonea tu. Walioiba ni watu waliokuwa wanajifanya wapo karibu na Kikwete, lakini Kikwete wa watu ni moja ya watu poa sana. Kikwete angetaka iba angekuwa moja ya tajiri mkubwa sana. Kwani kakaa serikali tena wizara nyeti kwa miaka mingi.

Tuache wivu wa kike, tumuache asafiri, anahitaji kumwakilisha rais ktk sehemu kadha wa kadha. Lakini pia Kikwete ana nyazifa bado za kimataifa huko. Na kusafiri uongeza kuishi kwa muda mrefu kwa msio tambua hilo.

EBU TUMWACHE RAIS KIKWETE APUMZIKE.
 
Nchi huliwa na wenye meno
 
Umeanza mapema kuchafua watu, kundi ulilonalo la 2025 jipangeni jinsi ya kuwatoa watu kwenye reli si kwa uzi huo ulioandika. Siku hizi kila kitu JK, akienda nje ya nchi hele kapewa na nani? Kawa waziri, Raisi awezi kendesha maisha yake kwa kipato chake? Huu mnyukano wa maslahi mepesi ndio unatupotezea mwelekeo.
 
Na yeye atuachie Nchi yetu ameshatunyonya vya kutosha atuache tuijenge nchi tuliyoachiwa na Mzalendo wa kweli, Mtetezi wa Wanyonge Mpinga ufisadi wa wazi wazi
 
Hivu Ni kweli kikwete Ni mbaya kiasi hiki?? Kama Ni kweli kikwete na washikaji zake Ni wabaya na wezi kiasi hiki..kwanini wasituhurumie..?
Hawa Wana mentality Ile ya kiarabu ya kuwa na sultan tokea dunia kuumbwa mpaka kiama. Kumbuka sultan said seyyid Koo yake bado no tajiri huko uarabuni na ndio hao hao wanatawala tokea biashara ya utumwa.
 
HAKUNA mkataba wa maana uliosainiwa na awamu ya Kikwete, viongozi wote waliokuwa wanasaini ile mikataba walikuwa wapiga dili. Kwa kweli Kikwete is the most useless President Tanzania has ever had.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…