Jambo lililopotoshwa sana, kuliko mengine

Jambo lililopotoshwa sana, kuliko mengine

chamilo nicolous

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2016
Posts
2,097
Reaction score
1,457
CHUKIZO LA UHARIBIFU NI UTENDAJI WA MAMLAKA YA KIBINADAMU KUPINGA AMRI NA MAMLAKA YA MUNGU
Unabii wa utendaji wa Chukizo la uharibifu lililonenwa na nabii Danieli umeandikwa katika Danieli 7, 8 na 9. Ni vipindi vitabu tofauti tofauti vya kihistoria ambavyo kanisa la Mungu lingelikabiliwa ma mateso yanayofanywa na mamlaka inayompinga Kristo.

1. Katika Danieli 7:25, kumetajwa unabii wa Wakati, Nyakati mbili na nusu wakati. Kipindi hiki kimerudiwa katika Ufun 12:14, sawa na miaka ya unabii 1,260, katika Ufun 12:6, au miezi 42 katika Ufun 13:5,6.
2. Katika Danieli 8:13,14, kumeelezwa unabii wa kipindi kirefu ndani historia ya Biblia, ambacho ni siku 2,300, ndipo huduma ya kutakasa patakatifu ianze.

3. Katika Danieli 9:22-27, kuna unabii wa wiki au majuma sabini, au miaka 490, ambapo mwishoni mwa wiki ya sitini na mbili, Masihi, yaani, Kristo angelikatiliwa mbali. Kipindi hiki kinahusisha ujio wa Kristo mara ya kwanza ili aifanye kazi ya upatanisho na kufa kifo cha msalaba. Kizazi cha mwisho cha unabii huo kingelikabiliwa na mateso ya kuharibiwa kwa mji wa Yerusalemu pamoja na hekalu, kama ilivyorudiwa na Yesu katika Marko 13:1-3, na injili ya Math 24 na Luka 21. Hii ndiyo awamu ya kwanza ya utendaji wa Chukizo la Uharibifu uliofanyika mwishoni mwa miaka 60BK , mji wa Yerusalemu ulipozungukwa na majeshi ya kipangani na kuwatesa na kuwauwa wote ambao hawakuzingatia masharti ya kujiponya yaliyoelezwa na Yesu katika Injili hizo. Katika Marko msisitizo wa masharti hayo umewekwa katika Marko 13:14-20.

KATIKA VIPINDI HIVI VITATU VYA UNABII WATU WAAMINIFU KWA MUNGU WANGELITESWA NA MPINGWA KWA NAMNA TOFAUTI TOFAUTI

1.Mateso haya ndiyo yamehusisha neno DHIKI KUU. Urefu wa MATESO ni tofauti kutegemeana na kipindi.

2.Unabii wa Chukizo la Uharibifu wa awamu ya pili ni ule wa ujulikanao kama, Wakati, nyakati mbili na nusu wakati mara mbili, au siku 1,260. Awamu hii ilitekelezwa na ufalme wa kirumi kwa kuungana na uongozi wa kabisa Katika, (lililojulikama zama hizo kwa jina la Roman Catholic-RC). Kwa pamoja serikali ya kirumi na uongozi wa kanisa hilo walitesa watu wa Mungu kwa kipindi cha miaka 1,260, kuanzia 538 hadi 1798AD. Lengo lilikuwa ni kuwazuia watu wasimwabudimu Mungu mwingine isipokuwa anayehubiriwa na kanisa hilo, siku ya inada ikiwa ni Jumapili.

3.Kwa mujibu wa unabii wa 2Wathes 2:1-5, na wa Ufunuo 13:11-18, tukio hili la MPINGA KRISTO, litajirudia miaka michache isiyozidi KIZAZI KIMOJA, kabla ya marejeo ya Kristo. Katika kipindi hiki cha mwisho, CHUKIZO LA UHARIBIFU litatekelezwa kwa kutumia UKENGEUFU, au MABADILIKO YA MAAGIZO YA AMRI ZA MUNGU. Mtekelezaji ameitwa, MTU WA KUASI, MWANA WA UHARIBIFU; AJIFANYAYE MUNGU, KWA KUKETI KATIKA HEKALU LA MUNGU ILI AABUDIWE YEYE BADALA YA MUNGU. Lengo litafanana na unabii wa siku 1,260. Wapingaji wa Amri zake watawekewa SHINIKIZO LA UCHUMI NA KUTAKIWA KUMWABUDU HUYO MNYAMA, AU NAMBA YAKE, ILIYO YA KIBINADAMU, (Ufun 13:15-18). Wenye kupinga watatezswa kwa kupitia DHIKI KUU AMBAYO HAIJAPATA KUTOKEA YA AINA YAKE, (Marko 13:20-23). Mwenye kujifunza unabii wa Daniel 7, 8 na 9, kwa kuulinganisha na jinsi unavyofunuliwa katika Ufunuo 10-13, atagundua kuwa utekelezaji wa CHUKIZO LA UHARIBIFU umegawanyika katika awamu kuu mbili; awamu ya pili ikiwa inajirudia kihistoria mara mbili. Wakati AWAMU YA PILI, (Sehemu ya 1), NI KIPINDI KIREFU CHA MIAKA 1,260, Sehemu yake ya pili haikupewa muda mrefu wa kiunabii. Kipindi kilichotajwa ni, tukio la ndani kizazi kimoja kisichomaliza muda wake,(Marko 13:19-23), kipindi ambacho kitahusisha ishara na maajabu mengi ya uongo kiasi cha kuwafanganya wengi wadhanie kuwa ni utendaji wa Mungu. Ijapokuwa kipindi cha marejeo ya Kristo, Biblia haitaji mwaka wala siku wala saa, kilichotajwa ni Kizazi kisichotakiwa kupita.

4. AMRI YA JUMAPILI NA ULAZIMISHAJI WA WATU KUMWABUDU MUNGU KATIKA SIKU YA KWANZA YA JUMA, NA VITISHO WA KUWAUWA WAASI WA AMRI HIYO, HAYO NI VIASHIRIA VYENYE KUFUNUA UTIMIAJI WA MWANZO WA KIZAZI CHA MWISHO. KIZAZI CHA MWISHO KILICHOTABIRIWA NA YESU KUWA HAKITAPITA KITATAMBULIWA NA WENYE KUFUATILIA VIASHIRIA VYA MATUKIO YALIYOELEZWA KATIKA VITABU HIVYO VYA BIBLIA. WASIOJIFUNZA UNABII WA BIBLIA KWA MAOMBI MENGI ILI WAELEWE UTIMIAJI WA UNABII HUU WATAKUTWA GIZANI.

TWAISHI KIPINDI GANI KWA SASA?
Mikakati inayoendeshwa na Serikali nyingi za dunia, unawaandaa watu kuishi kwa vitambulisho au Kadi maalumu, ambavyo vimelenga kuhakiki matumizi ya mali za raia wake. Pole pole kutatangazwa mambo ambayo yataweka shinikizo la uchumi.

Kwa mujibu wa agizo la Yesu la Injili ni lazima ihubiriwe kwanza kwa mataifa yote ndipo ule mwisho utakapokuja, ( Marko 13:10), walio waaminifu kwa Yesu watatumia mali zao kwa faida ya wokovu wao na wa wenzao, wakijihusisha katika kuihubiri injili, wakitumia fursa zitakazokuwa zinatumiwa na Mungu. Wenye moyo wa ubinafsi watakuwa wagumu kukubaliana na dhana ya kuwa tunakaribia kizazi cha mwisho. Wataitafsiri Biblia kwa namna iliyo tofauti ili kuwabakiza wengi gizani. Fedha zitageuzwa kuwa miradi muhimu ya walio watumishi ndani ya Kanisa, sawa na ilivyokuwa zama za Yesu na mitume. Kumhubiri Yesu kama Mwokozi wa ulimwengu kutapuuzwa. Vipaumbele vitawekwa kwenye mali kwa jina la mibaraka. Kuwauwa walio waaminifu kwa Mungu kutafanywa kwa kuwatuhumu kuwa wanajifanya kuwa watu wa Mungu, wakati kupitia kwa uongo wa wahubiri hao ulimwengu unapitia mambo magumu. Viongozi wa dini watashiriki kupiga kura ya kuwataka wahubiri waaminifu wauawe kuliko taifa lote kuangamizwa.

Uamuzi wa aina hii ulifanywa na Kuhani Mkuu ili kuidhinisha kifo cha Yesu. Hivyo Serikali za dunia zinapokazana kuweka michakato mipya ya uendeshaji wa kutawala watu na mali zao, watajikuta wakiwa na maridhiano na viongozi wa kidini. Hivyo tunapoyaona mambo yanayozidi kutushangaza, twatakiwa kujua kuwa muda siyo mrefu masharti mapya na yenye kuunganisha watu na mapenzi ya kidunia yatazidi kuonekana ni ya kawaida. Chukizo la uharibifu litaingizwa taratibu kwa werevu, kabila ya sheria ngumu kutekelezwa.

UNAJIANDAAJE KWA MAREJEO YA KRISTO MUDA SIO MREFU?
Warumi 13:11-14, pamoja na Waef 5:1-8, pamoja na Marko 13:32-37, na aya zingine nyingi zimetujulisha jinsi ya kuishi tukimgojea Yeye. Kila mmoja anategemewa amwamini na kumtii hata kama itabidi kifo cha kimwili kimpate. Atafarijiwa na kauli ya Ufun 14:13, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa, naam asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao kwa kuwa matendo yao yafuatana nao. Naomba Mungu anisaidie kuufikia mwisho wa Pambano kuu nikiwa mshindi, endapo ataniruhusu kulishiriki tukio la Chukizo la uharibifu lililo mbele yetu. Mshirikishe mwenzako ujumbe huu muhimu.(Muhtasari na Mch E.Kasika, 0764 151 346).
 
Back
Top Bottom