kihuba
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 264
- 265
[emoji830]Kuna jambo ambalo linawaangusha wafanyabiashara wengi na kuwafanya washindwe kufikia mafanikio
[emoji117]Jambo lenyewe ni *kutokuwa na subira,* Kwa mfano mtu unapongia katika biashara, na ukawauliza watu wenye uzoefu na biashara hiyo wakushauri ufanye nini ili upate mafanikio.Wakakushauri na Ukafanya na haukuona matunda, ukafanya tena na haukuona matunda, kisha utasema hii mbinu haifanyi kazi.
[emoji117]Kwa mfano umeambiwa sasa hivi kutangaza biashara yako mtandaoni kwa kutumia video utapata wateja wengi kuliko njia nyingine yoyote. Na ukarusha video ya kwanza ukapata views 2 au 3, ukarusha video nyingine ukapata views 10, Ukasema ngoja nilipie matangazo. Ukapata views 1000, watu wanacomment lakini hakuna mauzo.
Unarusha video nyingine unapata views 8000 lakini bado hakuna anayenunua.
[emoji117] Hapa kosa linalofanywa na wengi ni kuacha kutuma videos au kuacha kufanya anachofanya mara tu baada ya kuanza kama huoni matunda yake. Hili ndilo jambo linalowaua wajasiriamali wengi, watu hawana subira.
Kama wewe ni mjasiriamali wa aina hiyo unayeingia kwenye biashara unaanza kufanya vitu fulani ambavyo unajua ukiwa serious utapata matunda, lakini ukiona hakuna matunda ndani ya muda mfupi unaacha kufanya, Basi jambo linalokuangusha katika biashara yako ni kukosa subira.
[emoji185][emoji117] *Robert Kiyosaki* mwandishi wa kitabu *_ Rich Dad Poor Dad_* anasema “Usiache Kufanya Jambo kwa sababu umefeli, Acha kwa sababu umefanikiwa.”
Tuseme umepata fursa ya biashara, ukaamua kuifanya biashara hiyo, na hauna uhakika kama kweli unataka kufanya biashara hiyo. Lakini ukasema wacha nifanye hii biashara kwa muda fulani. Kwa hiyo kama utataka kuacha biashara hiyo basi usiache kwa sababu ya kufeli, ila acha kwa sababu umefanikiwa.
[emoji419]Kwa hiyo kama umeamua kufanya jambo hakikisha unaweka juhudi katika hilo.
[emoji830]Mfano kuna mjasiriamali mwingine anayeitwa *Mike Dillard* alipotaka kuanzisha podcast(makala sauti) alimuuliza mtu kwamba *“Nataka kuanzisha podcast, natakiwa kufahamu nini kabla ya kuanzisha.”* Yule mtu akamjibu “Kama haupo tayari kufanya podcast yako kila wiki kwa muda wa miaka mitatu mfululizo basi usianze.” Kwani utakuwa unapoteza muda wako.
[emoji419]Na ujumbe wangu kwa wajasiriamali wengine ni kwamba, Kama haupo tayari kusimamisha biashara yako kwa miaka mitato mpaka kumi ijayo basi achana na ujasiriamali. Kwa sababu kuna wakati utakaa mwaka mzima bila kuingiza chochote, kwa hiyo ni lazima ujiandae kwa hilo.
Hiki ni kitu muhimu sana cha kufahamu katika ujasiriamali. Sio kama wengi wanavyotangaza kwamba kama unataka maisha mazuri kuwa mjasiriamali, HAPANA, Kama unataka maisha mazuri kuwa mwajiriwa. Mafanikio ya mjasiriamali yanakuja baada ya miaka mitano ya mateso. Pia unatakiwa ukubali kwamba umeamua kuwa mjasiriamali unatakiwa upambane.
[emoji419]Pia unatakiwa ujue tofauti kati ya mwajiriwa na mjasiriamali, ajira unalipwa kwa kufanya kitu kilekile kila siku, lakini katika ujasiriamali unatakiwa kila siku ujihakikishie kuwa unafanya kitu bora zaidi kuliko ulichofanya jana. Kama upo kwenye mtandao na hupati wateja basi pengine kuna kitu hufanyi.
[emoji117]Kwa mfano, unaweza kuanzisha Instagram Channel na unaanza kupost kila siku.
[emoji666] Unajiwekea mkakati wa kufanya hivyo kwa muda wa miaka mitatu au mitano. Au unaamua kuanzisha YouTube Channel na unaamua kupost video 3 kila wiki kwa muda wa miaka mitano.
Hivyo hakikisha una subira katika kila unachofanya ili uweze kupata Mafanikio.