SI KWELI PreGE2025 Jambo TV wamechapisha taarifa kuwa John Heche amesema Gwajima Lengo lake ni urais kupitia CHADEMA

SI KWELI PreGE2025 Jambo TV wamechapisha taarifa kuwa John Heche amesema Gwajima Lengo lake ni urais kupitia CHADEMA

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)


IMG_20251001_103852_921.jpg
 
Tunachokijua
John Heche ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye alichaguliwa kutumikia nafasi hiyo Januari 21, 2025 akichukua nafasi ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Tundu Lissu ambaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Aidga Josephat Gwajima ni Askofu na mwanzilishi wa kanisa la 'Glory of Christ Tanzania Church' GCTC (Ufufuo na Uzima Ministries), kadhalika ni mwanasiasa ambaye mwaka 2020 alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM, ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Taifa (MNEC).

Siku za karibuni Askofu gwajima amekuwa mstari wa mbele katika kukemea vitendo vya utekaji pamoja na kutoa ushauri wa namna ya kukabiliana na vitendo hivyo. Pia ameshauri viongozi wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoingia kwenye Uchaguzi mkuu 2025 bila kushughulikia malalamiko yaliyopo miongoni mwa makundi mbalimbali ya wananchi.

Pia alishauri kufanyika kwa mabadiliko ya sheria (reforms) japo kwa uchache ili kuwezesha vyama vyote kushiriki uchaguzi mkuu wa 2025 na kuondoa migawanyiko nchini.

"Mnajua vyema kwamba Chadema wamesema hawaingii kwenye uchaguzi mpaka tufanye Reforms na modality yao wanayoisema, wanasema watazuia uchaguzi. "

"Tuamue kuwaruhusu hawa wa Chadema kuwapa reforms chache ambazo zinaweza kufanyika kwasasa, tuwape a minimal reform, haichukui muda. Tuwape, tuingie nao kwenye uchaguzi."


Taarifa inayomhusisha Gwajima na Heche


Kumekuwepo na grafiki inayodaiwa kuchapishwa na Jambo TV ikitumia sauti inayodaiwa kuwa ya John Heche kuwa amesema Askofu Gwajima haungi mkono 'No reforms No election' bali Lengo lake ni urais kupitia CHADEMA.

Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli bali ni ya kutengenezwa na wapotoshaji kwani haijachapishwa na Jambo TV kama inavyoonekana.

Changamoto katika muundo wa grafiki, matumizi ya fonti isiyotumiwa na Jambo TV ni sehemu ya mapungufu yanayodhihirisha taarifa hiyo kutengenezwa na wapotoshaji.

Pia kumbuka wapotoshaji wanaweza kunakilisha sauti za watu wasiohusika ikiwemo viongozi wa kisiasa, serikali, dini na kadhalika kutengeneza taarifa zisizo za kweli hivyo kuzua taharuki.
Back
Top Bottom