Jambo Usilolijua: Kambona -"Nyerere... Baba wa Taifa"; Hotuba yake tuliyoisahau

Mumpambe mtakavyoweza, kwangu mimi Oscar Kambona ni msaliti kwa Taifa hili, simtofautishi na EL, kiongozi mwenyeuchu na tamaa ya mali na utajiri wa haraka haraka.
Mali zake alijilimbikizia wapi?Ama ni yale yale ya sanduku la minoti mnalodai alikimbia nalo nje ya nchi?Kambona na EL wapi na wapi.
 
We don't think that was the case. Kambona failed to realize the timing on how to pass on his ideas, the point sometime is not being right or wrong but to be sure that you are doing something worthwhile at the right time and right place. Let us suggest that Kambona was right in terms of ideas, was it appropriate for him to do this within public domain. I conclude that both mheshimiwa Kambona and Mwalim Nyerere have done terrible mistakes in dealing with the matter, that's why it went out of control.
 
Maulaga,
Sikusema Kambona angeandika kwenye magazeti ya Tanzania, ingawa najua wakati alipoondoka alikuwa anamiliki gazeti la Mwananchi likiendeshwa na akina Gray Mattaka. Kambona angeweza kuandika kwenye magazeti ya Uingereza, magazeti ya Kenya kama vile Daily Nation na The East African Standard. Au angeandika tu kitabu. That is all I am saying.
 
Alisema....."Msingoje miaka mitano kama sifai - Msingoje. Mkipitisha azimio sasa hivi nitajiuzulu." Yaani, hii kitu ni kweli siku zote, zaidi zaidi sasa kwa kuwa tuna mijizi hii migamba.
 
Oscar Kambona on WikiPedia - http://en.wikipedia.org/wiki/Oscar_Kambona

Kambona hakuwa mtu mbaya, ndiyo maana alikuwa rafiki wa karibu sana wa Nyerere. Kama alivyodokeza MKJJ hapo juu ukichanganya kipande kingine cha historia yaani kesi ya uhaini, kuna uwezekano mkubwa sana kuwa mgogoro wao ulikuwa kwenye madaraka ambapo wote walikuwa articulate na mmoja wao akataka kupokonya mwingine
 
Hivi kwa Mwalimu Nyerere kuitwa baba wa taifa kunaisaidia nini Tanzania?
 
........Na yule Sykes........aliyemuandikia hotuba Nyerere na kuisoma UN.......naye tumuweke kwenye kundi lipi.................
 
........Na yule Sykes........aliyemuandikia hotuba Nyerere na kuisoma UN.......naye tumuweke kwenye kundi lipi.................
Abdulwahid Kleist Sykes hakumwandikia Nyerere hotuba aliyoitoa UN. Mohammed Said hapo kasema uwongo. Huenda ikawa Nyerere alitumia outline
ya mawazo ya Abdulwahid lakini Nyerere hakuwa mtu wa kusoma hotuba kama kasuku. Waulize wote waliofanya naye kazi watakuambia. And by the way, I happened to know Mzee Sykes in the days of my youth.
 
Hivi kwa Mwalimu Nyerere kuitwa baba wa taifa kunaisaidia nini Tanzania?

hehehe...umeona hilo ehhe? As if Tanganyika isingekuwa huru bila yeye! Give me a break...
Freedom was on the pipe no matter what...
Sijaona convincing evidence yeyote kuwa Nyerere single handed brought independence in Tz.
That said, it still good to appreciate him and give him his due rights and respects.
 
Inaelekea hii Kambona foundation inaweza kuwa na information kadhaa. Hopefully wanaweza kuweka vitu kadhaa wazi...
Mwingine wa kuangalia kwa karibu ni Sokoine. Some say his death was not a coincidence. Na since JKN was the president then, sidhani kama such organization would have been done w/out even his knowledge.
 
Mumpambe mtakavyoweza, kwangu mimi Oscar Kambona ni msaliti kwa Taifa hili, simtofautishi na EL, kiongozi mwenyeuchu na tamaa ya mali na utajiri wa haraka haraka.

hehehe! Mali na utajiri gani huo tena alitamani? Kusaliti taifa ni nini hasa? EL kasaliti taifa kivipi? Kama yeye amesaliti na chama chake kinachombeba kimesaliti pia? Na rafiki yake anayemuogopa?
 
Mumpambe mtakavyoweza, kwangu mimi Oscar Kambona ni msaliti kwa Taifa hili, simtofautishi na EL, kiongozi mwenyeuchu na tamaa ya mali na utajiri wa haraka haraka.
Na mimi hili ndilo lililonikwaza kwa Kambona wetu. Nilisoma pale Morogoro nikaonyeshwa jumba lake kubwa tu kwa viwango vya wakati huo. Hapa Dar nako kuna nyumba kadhaa zinahusishwa naye. Unajiuliza utajiri ule kwa umri na kazi za kuajiriwa alizofanya havikuendana kabisa. Kwa kuwa alioa Uchagani pengine hilo laweza kuwa jibu? Lakini mbona hata JS Warioba alioa huko na hakuwa tajiri? Hata Mkapa katajirikia Ikulu. Watawala wetu wengi walipenda kuoa Uchagani!
 
He is the symbol of our nationhood. He is the symbol of Tanzania in and out of Tanzania.
Mkuu, hivi leo ukipewa mtihani kuchora symbol ya Tanzania utamchora Nyerere au Karume?

Kweli mapenzi matamu, maana nasikia hata wananchi wa South Africa walitaka kuweka kiapo kiwe kwa jina la Mandela.
 
Kibatani cha thanks sikioni mkuu, ningekibofya.
 
Mkuu, hivi leo ukipewa mtihani kuchora symbol ya Tanzania utamchora Nyerere au Karume?

Kweli mapenzi matamu, maana nasikia hata wananchi wa South Africa walitaka kuweka kiapo kiwe kwa jina la Mandela.
Hata hizi alama kaziasisi yeye. Mwalimu ni kila kitu kwa uanzishwaji na uwepo wa TANZANIA.
 
Hata hizi alama kaziasisi yeye. Mwalimu ni kila kitu kwa uanzishwaji na uwepo wa TANZANIA.
Basi hata ushahidi hamna mkuu.

Ukitafuta, ndani ya JF, kuna topic inazungumzia shindano la jina Tanzania.
 
Basi hata ushahidi hamna mkuu.

Ukitafuta, ndani ya JF, kuna topic inazungumzia shindano la jina Tanzania.
Kasaini yeye kulikubali. Utaitaja wapi Tanzania umsahau Mwalimu? Historia haifutiki wala kuandikwa upya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…