Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza; Mvuvi Nigeria atafuna samaki mwenye thamani ya mabilioni ya shilingi bila kujua


Mtu mmoja nchini Nigeria amevua samaki aitwae Blue Marlin Fish mwenye thamani ya dola za kimarekani milioni 2.6 ($2.6 million) sawa na zaidi ya Shilingi Bilioni 6 za Kitanzania lakini bila kujua amemla yeye na wanakijiji wenzake.

Taarifa hiyo imesambaa zaidi kwenye mitandao ya kijamii baada ya jamaa huyo kushare picha ambazo zilionesha akiwa ametoka baharini kumvua samaki huyo lakini kwa sababu ya kutojua thamani yake wakaamua kumfanya kitoweo.


Blue Marlin Fish ni moja ya aina kubwa za samaki duniani ambao wanapatikana katika bahari ya kitropiki kama Atlantic na Pacific tu, na kwa bara la Afrika wanapatikana zaidi kwenye nchi za Africa Magharibi.

Aidha upatikanaji wao ni wa msimu hasa katika maeneo yenye joto na inasemekana ndani ya miili yao kuna aina ya madini ya Ruby na metali ya Zebaki ambayo matumizi yake ni kwenye mitambo na madawa.


Source:
A local Nigerian Fisherman captured a Blue Marlin Fish reportedly worth $2.6 million but ate it with his friends.
 
Kila nikitaka kujiambia sina bahati huwa nawakumbuka hawa jamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…