Uchaguzi 2020 Jambo wanalopaswa kufahamu CHADEMA, ni kwamba muda wa kufanya siasa za kistaarabu umekwisha

Mkuu hii njia mbadala ya kutafuta haki(vita) imewahi kuleta suluhisho la kudumu popote pale duniani???

Hii sio njia nzuri na kila mtu anaelewa hilo. Lakini inapokuwa ndio njia pekee basi hutumika. Na nchi nyingi za kiafrika zimepata uhuru wao kupitia njia hii. Hata Africa kusini weusi walipata usawa baada ya mapambano makali. kama maendeleo ni kipimo cha mtu kukaa madarakani basi huko Africa kusini ilitakiwa hao weupe wawe madarakani mpaka leo, na weusi wasubiri mpaka siku wazungu wakubali majadiliano. Huu muda unaopoteza hapa kakae kikao chenu cha ndani na wenzako uwaambie watii matakwa ya watu kupitia box la kura.
 
Asante
 
Acha kabisa kulinganisha Africa Kusini kupigania uhuru wao kutoka kwa Wazungu wachache na Tanzania ambayo ipo huru, huo mfano wako hauendani kabisa na Siasa za Tanzania maana kama ni uhuru tayari tulishakuwa huru miaka mingi sana nyuma.

Ninyi mnataka kuhalalisha "vita" ili kugombania "madaraka" na siyo kutafuta uhuru. Uhuru gani mnautaka wakati hili ni Taifa huru?? Kinachowasumbua ninyi ni tamaa ya madaraka ambayo Wananchi wamekataa kuwapeni sasa mnakuja na visingizio vya kijinga jinga ili mlete machafuko kwenye nchi yetu ya amani. Hakuna mtu atakayekubali kuwaachia mfanye kama mnavyotaka.

Fahamuni kwamba Serikali haiwezi kukaa kimya bila kuwashughulikia, na mtashughulikiwa kweli kweli, yaani mtapata tabu sana!
 
Siku cdm wakiongoza mapambano ya kutokea msituni nawahakikishia watapata uungwaji mkono mkubwa mnooooo.
 
Mr mkiki,,Ni bora ungeandika Uzi kwa kueleza mikakati kwa busara zaid ,huu upuuz unaondika unajua Athar zake ,,Ni Lin chadem walifanya siasa za kistaraabu ???plz over plz,Tumuombe mung Tusifike unakoona panafaa,,,,,,,,,,,huu Uzi moderator waundoe tu
 
Mr mkiki,,Ni bora ungeandika Uzi kwa kueleza mikakati kwa busara zaid ,huu upuuz unaondika unajua Athar zake ,,Ni Lin chadem walifanya siasa za kistaraabu ???plz over plz,Tumuombe mung Tusifike unakoona panafaa,,,,,,,,,,,huu Uzi moderator waundoe tu

Siasa za kistaarabu ni zipi ?.Yani nikikumbuka mlivyo mtukana Mh Lowasa ktk Uchaguzi Mkuu wa 2015 nnaona kinyaa Maneno yako kabisa.
 

Kwa sasa nimegundua naongea na mtoto asiyejua lolote zaidi ya kubebeshwa propaganda za kitoto. Kwa taarifa yako Africa kusini imepata uhuru wake 1930. Walichofanya hao weusi ni kupigania kuondoa ubaguzi wa rangi. Kama ni uhuru basi hao wazungu wangeondoka.

Hapa nchini pia watu hawapiganii uhuru bali wanataka kuitoa ccm madarakani kwa njia halali ya box la kura. Lakini umoja wenye nia ovu baina ya ccm na vyombo vya dola ndio unapelekea box la kura kutokuheshimiwa, na ushahidi wa box la kura kutokuheshimiwa ni watu kutokupiga kura. Katika mazingira ya box la kura kutokuheshimiwa basi mleta uzi kaja na wazo sahihi la kuwatoa kwa njia ambayo itafanya box la kura kuheshimiwa baada ya kutiana adabu.
 
Mkuu umeandika mengi lakini uchache wa wapiga kura unaweza usiwe na tatizo kama ahadi zinazotolewa zinatekelezeka.

Kumshawishi mtu aende kupiga kura, wakati mwingine kunachangiwa na uwepo wa vitu tangible vinavyofanyika.

Ilitolewa ahadi ya matrekta 10 pale SUA, imetekelezwa.

Ilitolewa ahadi ya manunuzi ya ndege, zinaendelea kuja.

Ujenzi wa fly overs unaendelea na madaraja mengine mengi tu.

Meli zinaanza kufanya kazi kwenye maziwa tuliyojaliwa na Mungu.

Yanayofanyika ni mengi sana, na uchache wa watu huko Buyungu sio kigezo kwamba 2020 idadi itapungua kulinganisha na 2015.

Upinzani ubadilike, kulialia mitandaoni hakuna msaada wowote ule zaidi ya kujiongezea hasira zenye kuleta magonjwa kama zile cancer.
 

Mkuu sikujua kwamba hujui maana ya ushindani ni nini? Ni nani aliyekuambia hayo mambo uliyotaja yakitekelezwa ndio unapata uhalali wa kulazimisha kubaki madarakani? Kama ni hivyo nchi zenye maendeleo duniani si ingekuwa chama kimoja tu ndio kiko madarakani mpaka leo? Kumbuka hayo mambo chama chochote kinachoingia madarakani kinapaswa kuleta maendeleo kwani ndio kinachoratibu kodi za wananchi. Kila chama kiklichoko madarakani kina wajibu wa kuleta maendeleo ili mradi kinakusanya kodi, lakini hilo halitoi uhalali wa kulazimisha kubaki madarakani bila ridhaa ya wananchi, kwani hata vyama vingine navyo vinaweza kuleta hayo maendeleo kwa mtindo (sera) wao. Ingekuwa hela za maendeleo hutoka kwenye mifuko binafsi ya wanachama wa chama kilichoko madarakani hoja yako ingekuwa na mashiko.
 
Unadhani hii nchi ni île ya tanu n'a asp ,Na nyerere ? Au bado unakaa les shemejii ?
 
jino kwa jino. Tumechoka mkuu
 
Ushindani upo, lakini yapo mengi tu ambayo ni adui wa maendeleo ya nchi za kiafrika yanayojificha kwenye huo huo ushindani. Vyama vingi viwepo lakini nchi isiingizwe kwenye anarchy kwa kigezo cha demokrasia.

Watu waache kuwekeza kwenye ujasiriamali na kilimo waende kukaa juani kuwasikiliza wanasiasa kwa kigezo cha demokrasia na ushindani.

Hao walioutuletea huo ushindani hawana siasa za bei rahisi kama zetu. Wanamaliza uchaguzi na akili zao zote zinahamia kwenye uzalishaji mali.

Sisi huku tunadanganya kuwa siasa za kweli ni za kutembea nchi nzima na kufanya mikutano january mpaka desemba. Hakuna kitu kama hicho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…